THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

Gadget

This content isn't available over encrypted connections yet.

BONANZA LA MICHEZO KUADHIMISHA SIKU KUU YA NANE NANE.

Timu ya mpira wa miguu ya Efm redio ilishika ushindi katika Bonanza la michezo ambalo liliandaliwa na uongozi wa shule ya Baobab ambapo timu mbalimbali za mpira wa miguu zilishiriki ikiwemo Boko Veterani, Bunju Veterani, Bukurumawe F.C, Migude Veterani pamoja na timu ya shule ya sekondari baobab.

Akizungumza katika mashindano hayo Mgeni rasmi Diwani wa Kata ya Mpinga alisema “Efm redio imekua ikionyesha ushirikiano kwa kucheza michezo mbalimbali ikihusisha jamii inayoizunguka kwani ni njia moja wapo ya umoja na mshikamano. Vilevile aliwapongeza uongozi wa shule ya sekondari Baobab kwa kuandaa bonanza hilo kwani michezo huimarisha afya.
Kikosi cha Timu ya Efm wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kushinda Mbuzi katiika mchezo wa mpira wa Miguu katika maadhimisho ya siku ya Nanenane.