THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

Gadget

This content isn't available over encrypted connections yet.

BREAKING: Jenerali Ulimwengu apata ajali ya gari, akimbizwa Moi

Taarifa iliyotufikia inaeleza kuwa, Mwandishi Mkongwe nchini na Mwenyekiti wa Bodi ya Gazeti la Raia Mwema, Jenerali Ulimwengu amepata ajali mapema asubuhi ya leo, na kupelekwa hospitali ya Taifa ya Muhimbili kitengo cha mifupa Moi kwa matibabu. 
Ajali hiyo imehusisha gari alilokuwa akiendesha yeye aina ya Benz na gari nyingine iliyoigonga gari hiyo upande wa Ubavuni.

Mwandishi mkongwe Jenerali Ulimwengu akijuliwa hali na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Paul Makonda katika  Taasisi ya Tiba ya Mifupa Muhimbili (MOI) Dar es Salaam ambako amelazwa kwa matibabu baada ya kujeruhiwa katika ajili iliyotokea Mikocheni, Dar es Salaam.

Gari alilokuwa anatumia mwandishi mkongwe Jenerali Ulimwengu baada ya ajali hiyo.


Hoja moja imeshachangiwa mpaka sasa.

  1. Sufa Anasema:

    Nakutakia speed recovery mwanamapinduzi Taifa zima bado linahitaji mchango wango muhimu. Pole sana!