THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

Gadget

This content isn't available over encrypted connections yet.

TANZIA: MALKIA WA TAARABU SHAKILA SAIDI AFARIKI DUNIA JIJINI DAR ES SALAAM LEO

Habari za kusikitisha zimetufikia muda huu kuwa malkia wa Tarabu nchini Bi. Shakila Saidi amefariki dunia jioni ya leo muda mfupi baada ya kuanguka na kukimbizwa hospitali ya karibu na nyumbani kwake Mbagala Charambe jijini Dar es salaam. 
Kwa mujibu wa Rais wa Shirikisho la Muziki Tanzania Bw. Addo November, Bi Shakila hakuwa anaumwa ila baada ya kumaliza kuswali alianguka ghafla na alipofikishwa hospitali alikokimbizwa  alikutwa amekwishafariki. Taarifa kamili  ya mipango ya mazishi 
tutawaletea mara tu tutapozipata.
MOLA AILAZE PEMA ROHO YA MAREHEMU - AMINA
------------------------------
Kipindi cha DANGA CHEE cha MICHUZI TV kilipata bahati ya kuongea na marehemu Bi Shakila enzi za uhai wake takriban miezi sita iliyopita.
Sikiliza mahojiano hayo hapa chini:


Kuna Maoni 3 mpaka sasa.

 1. HK Anasema:

  La Hawla Wala Quwwata Illa Billah.
  Inna Lillahi Wainna Ilayhi Rajiun. poleni sana wafiwa wote na wote mliokhusu msiba huu.
  Mwenyeez Mungu amrahamu amughufirie kwa yote na amlaze pema peponi anapostahili na kesho awe miongoni mwa waja wake wema watakaoingia katika yake Firdaus. - AMEN. Maskini Bi Shakila Saidi hatunae tena na alitamani sana japo siku moja aje aimbe na Nasib Abdul (Diamondo Platnumz) pia alitamani sana akutane na Mh. Rais John Pombe Joseph MAGUFULI, sina hakika kama alijaaliwa kuyafanikisha yote hayo, lakini yote ni mipango yake Mwenyeez Mungu. Hakika wapenzi wake wote wa muziki wa Taarab, khususan Taarab asilia, tutamkumbuka sana Bi Shakila Saidi katika nyimbo zake na khasa sautiye maridhawa aliyokuwa kajaaliwa, Masha Allah.

  Yaani kama kuna uwezekano wowote kwa Diamond Plutnumz, itabidi hii nyimbo "Macho yanacheka Moyo Unalia.." Diamond Plutnumz hii nyimbo fanya kila hali alau uje uiimbe japo na mwanawe Bi Mwape Kibawana kama ataridhi. Iwe ni katika kumuenzi Mama yake kama alivyotamani sana kuiimba na wewe nyimbo hiyo, lakini MOLA hakulijaaliya hilo. Pumzika Pema Peponi Mama yetu Bi Shakila Bint Saidi.

 2. Anonymous Anasema:

  M.A.P Bi.Shakira....

 3. Anonymous Anasema:

  Ningefurahi sana na moyo wangu kutulia nitakaposikia mheshimiwa rais amehudhuria mazishi ya huyu mama alikadhalika Daimond nae afanye lile alilokua akilitamani huyu mama. R.I.P