Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof.Makame Mbarawa amemsimamisha kazi Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Ndege Tanzania (ATCL), Mhandis  Johnson Mfinanga na Mkurugenzi wa Uendeshaji, Captain Sadick Muze kwa kosa la  kuchagua rubani mmoja ambaye hajakidhi vigezo anavyotakiwa kuwa navyo marubani wanaotarajia kuondoka kesho kuelekea nchini Canada kwa  ajili ya mafunzo  ya kurusha ndege mpya mbili zinazotarajiwa kuwasili nchini katikati ya mwezi Septemba.

Akizungumza na waandishi wa habari wilayani Kyela, Mkoani Mbeya Prof. Mbarawa amesema baada ya kukamilisha malipo ya awali ya ununuzi wa ndege mbili mpya kwa ajili ya ATCL  alitoa maelekezo kwa Kaimu Mkurugenzi Mkuu huyo kuwachagua marubani watano wenye vigezo ambavyo vinahitajika kwa ajili ya mafunzo hayo jambo ambalo amebaini mmojawapo wa waliochaguliwa hajatimiza vigezo na hivyo kuamua kumsimamisha kazi kwa kosa la uzembe.
Waziri  Mbarawa amesisitiza kuwa msimamo wa serikali ni kuhakikisha kila mtumishi  wa umma anatekeleza wajibu  wake kwa kufuata sheria kanuni na taratibu hivyo atakaye kiuka msimamo huo Serikali haitasita kumchukulia hatua za kinidhamu.
Shirika la Ndege Tanzania katika mwaka huu wa fedha Serikali imetenga kiasi cha shilingi bilioni 500 kwa ajili ya ununuzi wa ndege tatu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 10 mpaka sasa

  1. Sawa sawa kabisa, hamna uzembe kwenye serikali hii, kuchagua watu kwa kujuana ambao hawana sifa. Sasa baaasi. Hapa kazi tu. Ahsante Ndugu Magufuli kwa kuweka nidhamu kazini.

    ReplyDelete
  2. Wabongo hulka yetu ni kufurahi popote pale tunapoona mtu anashindwa ama anaadhibiwa. Hatufurahii mafanikio ya watu. Ajabu sana.

    ReplyDelete
  3. The mdudu, #mazoea mabaya sana haya mtu mzima limemkuta kwa uzembe wa kijinga kabisa ndio maana kumbe Air Tanzania yetu ilikua kama mtoto alie bemendwa kwa upumbavu kama huu Asante sana serikali ya awamu ya 5 chini ya Rais wetu mpendwa John Pombe Magufuli na serikali yote kwa ujumla #hapakazi2

    ReplyDelete
  4. Huyoo n engn sio capt mfinanga...

    ReplyDelete
  5. CEO n engn sio capt

    ReplyDelete
  6. Bwana Mfinanga ni Mhandisi (Engineer) na si Rubani (Captain)....Mie nakubaliana na uamuzi wa Mheshimiwa Waziri,Hakuna tena nafasi ya ujanja ujanja wakati wa kufunga. ATCL imekuwa shamba la bibi kwa muda mrefu sana ni wakati wa kufanya kazi sasa.Mdau hapo juu unatetea na kusema hulka?Sijui wqtanzania tu nataka jened,Huko nyuma mlisema uongozi ilikuwa soft sana sasa mnatetea uozo!Hii Serekali ya kazi sio mzaha mzaha,miezi nane tu toka JPM aanze kazi jana report ya IMF imeonyesha Tanzania inaongoza kwa uchumi kwa nchi za Africa ya mashariki.Hapa kazi tuuuu

    ReplyDelete
  7. Bora Mh. Waziri kalibaini hilo mapema, maana huko usoni pangelikuja kubainika udhaifu wowote kuhusiana na hilo, Mh. JPM hana cha msalie, mara unakuta anamtumbuwa Mh. Waziri mwenyewe. Juu ya hilo tunampongeza Mh. Waziri kwa umakini wake katika kuwajibika na pia iwe fundisho kwa watendaji wengine katika sekta zao mbali mbali, tukumbuke zile zama za kuangalia...'WHO' zimeshakwisha, sasa ni mwendo wa kuangalia na kupima 'HOW'. Kila la kheri Tanzania yetu mpya katika gea ya HAPA KAZI TU!

    ReplyDelete
  8. Wewe mdau wa pili akili yako ipo namna gani sijui. Mtu anafanya madudu wazi wazi halafu unasema wabongo wanafurahia. Ameshapewa onyo wote kwenye mashirika ya uma na serikalini na bado unafanya makosa yale yale. Ni kama vile unakwenda kulewa kwa pesa zako mwenyewe halafu unaenda kujikojolea kitandani halafu mkeo akae kimya tuu. Wewe vipi. Nchi inabadilika na watu bado wanaendelea na uzembe.

    ReplyDelete
  9. Sasa wewe unyesema WaTanzania waafurahia mtu anaposhindwa ndio mTANZANIA HATARI SANA! Je huyo mtu angeenda huko akakutana na WaZungu makini wakamrudisha kwa kutokuwa na uwezo ndege ungeenda kurusha wewe?. Nani angelipa hiyo hasara? Unaweza kufikiria consequnces zake?

    ReplyDelete
  10. Mtu anakuwaje rubani halafu anakuwa hana sifa ? manake maelezo yako general sana.tungeambiwa labda training ya macaptain labda akapelekwa Junior Officer au training ilihitaji rubani mwenye masaa kadhaa wakaachwa wenye masaa mengi wakapelekwa wenye machache.Navyojua mm mi pilot wazuri wengi sana wameondoka ATCL kwa sababu Shirika halina muelekeo

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...