Taarifa iliyotufikia mchana huu, inaeleza kuwa  kuwa Rais wa awamu ya pili wa Zanzibar na Mwenyekitiwa Baraza la Mapinduzi (1972-1984), Mzee Aboud Jumbe Mwinyi amefariki dunia leo baada ya kuugua kwa muda mrefu. Alikuwa na umri wa miaka 96.
Mzee Aboud Jumbe amefikwa na mauti hayo nyumbani kwake Kigamboni, Jijini Dar es salaam. Rais wa Jamhuri wa Muungano amemtumia Salaam za rambirambi Rais wa Zanzibar na Mwenyekti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein kwa msiba huu mzito

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Poleni wafiwa mnapoomboleza kifo cha mzee huyu aliyewahi kuongoza Zanzibar

    ReplyDelete
  2. RIP Mzee Aboud, Polen sana familia pamoja na Taifa kwa ujumla kwa msiba huuu.

    Swali tu, tukisema Serikali haina dini kwa maana ya imani; mbona barua toka Kurugenzi ya mawasiliano ya Ikulu imeweka maneno ya Inna lilahi wa inna ilaihi rajiun? Je nimekosea au wamekosea? Ni swali jema tu na ningependa kuelimishwa toka kwa wataalam na wajuzi wa haya mambo (Protocol).

    Asante

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...