THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

DALADALA LAPINDUKA KITUONI MBAGALA-SABASABA JIJINI DAR ES SALAAM, WATU KADHAA WAJERUHIWA

DALADALA lenye namba za usajili T274 DEX, lililokuwa likifanya safiri zake kati ya Mbagala RangiTatu kuelekea Temeke jijini Dar es Salaam, limepiga mweleka mita chache tu kutoka kituo cha Daladala Sabasaba-Mbagala mapema leo asubuhi (Agosti 11, 2016) na kujeruhi watu kadhaa.

Mashuhuda wanasema, Daladala hilo lililokuwa katika mwendo kasi, liliserereka na kuacha njia wakati likikaribia kusimama kituoni hapo.
Dereva wa Daladala hilo aliruka na kukimbia, nakuwaacha abiria wakitaharuki kila mmoja akijaribu kukoa maisha yake.

“Unajua mvua hizi zilizonyesha asubuhi zinafanya barabara iteleze na hawa jamaa mwendo wao unajua tena, sasa alijaribu kufunga breki gari likaanza kuserereka na alipojaribu kurudi barabarani likakataa na kutumbukia mtaroni,” anasimulia mmoja wa mashuhuda aliyekuwa eneo la ajali.
Polisi wa usalama barabarani alifika muda mfupi baada ya ajali hiyona taratibu ya kuliondoa gari hilo zilianza.

Abiria wote walitoka salama, wachache walijeruhiwa na baadhi yao walionekana wakilia kutokana na mshtuko wa ajali hiyo ya asubuhi.
 Mtu huyu ambaye haikujulikana maramoja kama ni muhudumu wa daladala hilo au abiria akitoka ndani ya daladala hilo baada ya "kupiga mwereka'
 Mashuhuda kama kawaida yao
HABARI/PICHA NA K-VIS BLOG/KHALFAN SAID
  Mmoja wa abiria aliyenusurika akilia kwa huzuni kutokana na ajali hiyo
 Wapita njia wakimuuliza abiria huyu (aliyekaa), ambaye alikuwa ndani ya daladala hilo.