Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Miraji Jumanne Mtaturu akizungumza na wananchi wa kijiji cha Mang’onyi wakati wa kutatua mgogoro kati ya wananchi na muwekezaji Shanta Gold Mine.
Wananchi wakielemishwa na Mkuu wa wilaya juu ya siasa zinazokwamisha maendeleo yao huku wanasiasa wenyewe wakishindwa kufanya uwakilishi katika maeneo yao badala yake wamekuwa wawakilishi wa kitaifa
Msingi wa kikao ni kusikilizana Mkuu wa Wilaya ya ikungi Miraji jumanne Mtaturu, Kamati ya ulinzi na usalama Wilaya, Uongozi wa Shanta Gold Mine na wananchi Kijijini Mang’onyi wakiwa kwenye mkutano wa kutatua mgogoro wao

Na Mathias Canal, Singida

Mgogoro uliodumu katika kipindi cha zaidi ya miaka kumi kati ya wananchi wa Kijiji cha Mang'oni na Muwekezaji Shanta Gold Mine umechukua sura mpya ya maelewano baada ya wananchi kupatiwa elimu kuhusu umuhimu wa uwekezekezaji na fursa watakazozipata ikiwa ni pamoja na ajira kwa wananchi wenyewe na maendeleo ya Vijiji, Kata, Tarafa, Wilaya, Mkoa na Taifa.

Akiwa katika kijiji cha Mang'onyi, Kata ya Mang'onyi Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu amezungumza na wananchi hao kujua kadhia iliyopelekea kutoelewana kwa kipindi chote hicho jambo ambalo limerudisha nyuma maendeleo tarajiwa kwa pande zote mbili.

Mgogoro huo umemalizika kwa Mkuu huyo kuamua kuwa wananchi walipwe fidia haraka iwezekenavyo ili kupisha uanzishwaji wa Mgodi huo ambapo tayari takribani wananchi 67 watalipwa katika awamu ya kwanza huku wengi zaidi 130 kulipwa katika awamu ya pili.

Dc Mtaturu amefanya mkutano wake wa hadhara wa mwanzo tangu ateuliwe kuwa Mkuu wa Wilaya ya Ikungi ambapo amewaagiza wawekezaji hao kukutana na kuwa na kikao cha pamoja kati yao na wananchi waliofanyiwa tathmini kwa ajili ya makubaliano ya namna bora ya malipo yao ikiwa ni pamoja na kuwashauri kila mmoja kufungua Account Bank ili iwe rahisi na salama katika uhifadhi wa fedha zao.

Baadhi ya Wananchi katika kijiji hicho cha Mang'oni hivi karibuni walizuia njia kwa kuweka magogo na mawe barabarani kama ishara ya kuwazuia wawekezaji hao kupita katika eneo lao kwa madai ya kutolipwa fidia kwa wakati na mwekezaji kuweka alama za mipaka ya eneo lake pasina wananchi kushirikishwa.

Hata hivyo Dc Mtaturu alisema kuwa huenda wananchi walikuwa na hoja ya msingi lakini kutolipwa fidia hakumfanyi mtu kupata uhalali wa kuharibu mali za muwekezaji kwani kufanya hivyo ni sehemu mojawapo inayochelewesha ulipaji wa fidia.

Mtaturu ameonyesha kukerwa na viongozi wanaowapotosha wananchi hao ilihali wakiwa wamejificha ama wanaishi mbali na kijijini hapo na kusema kuwa hiyo ni nidhamu ya woga kwani muwakilishi mzuri wa wananchi ni yule anayetanguliza maslahi ya wananchi mbele kuliko masalahi ya kisiasa, Chama ama maslahi yake binafsi.

Mkuu huyo wa Wilaya amesema kuwa kiongozi mzuri daima ni yule anayetatua changamoto za wananchi sio kuzipinga kwani siasa safi na nzuri ni ile inayoleta maendeleo sio kupinga maendeleo.
Amewataka wawekezaji hao kuwa na mahusiano mazuri na wananchi kwani unapokuwa na mradi wako katika Kijiji chochote nchini usipokuwa na mawasiliano mema na wananchi wa eneo husika ni dhahiri kuwa mradi wako utakuwa hauna tofauti na mradi mfu.

Hata hivyo pamoja na faida kwa wananchi kulipwa fidia na serikali kupata pato lake lakini wananchi 60 kutoka Kijijini hapo wataajiriwa katika Mradi huo kati ya ajira 120 zilizopo ambapo wengine 60 watatoka nje ya eneo hilo ili kutoa fursa kwa watanzania wote kujipatia ajira.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...