Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, jinsia, wazee na watoto, Dkt. Kigwangalla, jana jioni aliendesha Operesheni Maalum ya ukaguzi wa ofisi za shirika lisilo la kiserikali la Community Health Education Services and Advocacy (CHESA), ikiwa ni muendelezo wa vita ya uhamasishaji wa vitendo vya mapenzi ya jinsia moja ulioanza kuota mizizi nchini. 

Shirika la CHESA, pamoja na Mashirika mengine (majina yao kapuni) yanadaiwa kuendesha shughuli ambazo ni tofauti na zile walizosajiliwa kufanya, ikiwemo tuhuma za kuhamasisha watu wanaofanya mapenzi ya jinsia moja kudai haki zao kupitia miradi yao na harakati nyingine mbalimbali. 

Mashaka yametanda kwenye nchi nyingi Africa, kuwa kuwa nchi nyingine ambazo zihusiana na marafiki zetu wanaoruhusu mambo haya kwenye sheria, mila na desturi zao kuanzisha mikakati ya kichini chini ya kusambaza pesa kwenye vikundi mbalimbali vya kijamii na asasi zisizo za kiserikali ili kuwahudumia, kuwaunga mkono, kuwaunganisha, kuwatetea, kuwalinda, kuwawezesha, na kuhamasisha jitihada za siri sana na makini za kueneza mapenzi ya jinsia moja nchini.  Pia kuhalalisha kama utamaduni Mpya kwa kisingizio cha haki za binadamu. 
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, jinsia, wazee na watoto, Dkt. Kigwangalla akiongozwa kuingia ngani ya ofisi ya shirika lisilo la kiserikali la Community Health Education Services and Advocacy (CHESA), linalodaiwa kuendesha shughuli ambazo ni tofauti na zile walizosajiliwa kufanya, ikiwemo tuhuma za kuhamasisha watu wanaofanya mapenzi ya jinsia moja kudai haki zao kupitia miradi yao na harakati nyingine mbalimbali.

Tanzania imesaini mkataba wa kimataifa wa haki za binadamu (International Bill of Rights) lakini kwenye mkataba huo Hakuna kipengele hata kimoja kinachoelezea uwepo wa Haki zinazodaiwa na kundi hili. 

"Serikali itaendesha harakati nzito za uchunguzi wa pesa zote zinazoenda kwenye NGOs Na vikundi mbalimbali na kufuatilia pesa hizo zimeenda kufanya nini kwenye jamii." Alisema Dkt. Kigwangalla. 

"Nimewapa agizo wataalamu kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kushirikiana na jeshi letu la polisi kufanya kazi hiyo na kuyafikisha mahakamani Mashirika yote yatakayokutwa na hatia na pia kuchukua hatua ya kuyafutia usajili mashirika yote yatakayobainika kukiuka masharti ya usajili wao kwa mujibu wa sheria. Kwa mfano, coincidentally, tayari shirika hili litapaswa kutoa maelezo juu ya pesa lilizopokea kutoka shirika la kimataifa la JHPIEGO kutekeleza mradi wa SAUTI, ambao kwenye taarifa zake za mwaka limezificha. Mradi wa SAUTI unahudumia watu wanaofanya mapenzi ya jinsia moja." Aliendelea kusema Dkt. Kigwangalla. 
Shirika la CHESA kwenye usajili wake hakuna mahali linaeleza kwenye Katiba inayolianzisha kuwa litatoa huduma hizo. Na sababu ni rahisi, kwamba lisingeweka huduma hizo kwa kuwa lisingesajiliwa. 

Miaka ya hivi karibuni Serikali ilifuta usajili wa NGO moja iliyojulikana kama 'Sisi Kwa Sisi' Kwa tuhuma kama hizi. Kwenye uchunguzi huu, imebainika kuwa baadhi ya viongozi wa iliyokuwa Sisi Kwa Sisi ni waandamizi kwenye CHESA. Je, Sisi Kwa Sisi Siyo CHESA kwenye rangi nyingine? 
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, jinsia, wazee na watoto, Dkt. Kigwangalla akizungumza na baadhi ya watendaji wa shirika lisilo la kiserikali la Community Health Education Services and Advocacy (CHESA), linalodaiwa kuendesha shughuli ambazo ni tofauti na zile walizosajiliwa kufanya, ikiwemo tuhuma za kuhamasisha watu wanaofanya mapenzi ya jinsia moja kudai haki zao kupitia miradi yao na harakati nyingine mbalimbali, wakati alipolitembelea shirika hilo jana.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, jinsia, wazee na watoto, Dkt. Kigwangalla akiangalia moja ya vyeti vya  shirika hilo la CHESA, linalodaiwa kuendesha shughuli ambazo ni tofauti na zile walizosajiliwa kufanya, ikiwemo tuhuma za kuhamasisha watu wanaofanya mapenzi ya jinsia moja kudai haki zao kupitia miradi yao na harakati nyingine mbalimbali.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 7 mpaka sasa

  1. Mheshimiwa, hiyo bendera ni ya watu wa LGBT. Inakuwa na rangi ya Rainbow.

    ReplyDelete
  2. Mheshimiwa hao ni wale wale tu wanaofadhiliwa na serikali za ki magharibi kutuharibia kizazi ,angalia vizuri hapo Chini utaona bendera yenye rangi za homosexuality, lazima wafaham Kuwa sisi sio wao, wasitulazimishe kama vile wao wasivyopenda kulazimishwa. Futa usajili wao kabisa.tuna mengi ya kufanya,njaa,umasikini,maradhi,elimu.makazi bora,kilimo bora yote yanatusubiri.hao ni wabinafsi wasaliti wapenda matumbo yao wako tayari kuwasaliti watanzania kwa maslahi yao.
    Mdau kutoka Bukoba.

    ReplyDelete
  3. TWILA KAMBANGWAAugust 16, 2016

    mjomba Hamisi kabendela hako hapo hawana cha kujitetea kabisa, fungia toa mbio

    ReplyDelete
  4. Mheshimiwa bendera hiyo ni ya watu wanao amini ktk ushoga na ndoa za jinsia moja ulimwengu mzima unajua, kick them out .angalia free Wikipedia kwa maelezo zaidi
    https://en.m.wikipedia.org/wiki/LGBT_symbols

    ReplyDelete
  5. wanalazimisha ushenzi wao kwa waafrica,
    waziri endelea kuwatumbua,
    kinachokera magay wa bongo ni malaya wauza miili,
    shida za miasha zimewafanya wauze matako,
    na haya mashirika yanasema haki za binadamu ipi hiyo?
    ya umalaya kuuza matako?
    bongo hakuna gay ni machangudoa wa kiume

    ReplyDelete
  6. Asante Mheshimiwa kwa kulivalia njuga hili, nina imani hujachelewa. Umma tuko nyuma yako/yenu. Mungu awalinde.

    ReplyDelete
  7. HUKO NJE WANA MIHELA YA KUMWAGA TU. WANATUMIA HAYO MAHELA YAO KUVULUGA DUNIA NA KUTANGAZA USHETANI. kWA NINI WASSITUMIE MAPESA HAYO KUTUNUNULIA MADAWATI, MAJENGO YA SHULE, UMEME, MABARABARA, ELIMU YA AFYA NK!!!!!!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...