Taasisi ya Dr. Amon Mkoga Foundation imetoa msaada wa madawati 90 yenye thamani ya shilingi milioni 5.5 kwa shule za msingi katika manispaa ya Tabora, ikiwa ni mchango wa Taasisi hiyo katika kuisaidia serikali kukabiliana na upungufu wa madawati katika shule za msingi nchini.

Akizungumza leo katika hafla ya makabidhiano iliyofanyika katika ofisi ya mkuu wa wilaya Tabora mjini , Mwenyekiti wa Taasisi hiyo, Amon Mkoga amesema mchango huo ni sehemu ya utekelezaji wa dhamira ya taasisi hiyo ya kuunga mkono jitihada mbalimbali za kuleta maendeleo nchini.

“Mchango huu ni sehemu ya jitihada mbalimbali zinazofanywa na Dr. Amon Mkoga Foundation katika kusaidia utekelezaji wa miradi yenye tija kubwa kwa jamii. Tunaamini kwamba kupitia msaada huu, Taasisi yetu inatoa mchango wake katika kujenga viongozi wa baadaye wa taifa hili na wanataluuma mbalimbali wakiwamo madaktari, wahandisi na wengineo, “amesema Mkoga.

Makabidhiano yalihudhuriwa na Afisa Tawala Wilaya ya Tabora mjini, Sweetbert Nkuba ambaye alisema madawati hayo 90 yataboresha mazingira ya kujifunzia kwa watoto katika Mkoa wa Tabora na kutoa wito kwa wadau wengine kuunga mkono zoezi hilo.
Afisa Tawala Wilaya ya Tabora mjini, Sweetbert Nkuba (kushoto) akipokea moja ya madawati 90 yaliyotolewa na Taasisi Dr. Amon Mkoga na kukabidhiwa kwake na Mwenyekiti wa Taasisi hiyo Ndg. Amon Mkoga (kulia). Anayeshuhudia ni Mkuu wa Kitengo cha uhusiano na Uhamasishaji wa Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii (SSRA), Bi. Sarah Kibonde Msika ambao ni wadhamini wa kampeni hiyo iitwayo “Simama Kaa”
Sehemu ya Wanafunzi wa shule za msingi katika manispaa ya Tabora wakiwa na madawati hayo.
Mwenyekiti wa Taasisi hiyo Ndg. Amon Mkoga akiwa na baadhi ya wanafunzi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Kuchangia maendeleo ni kitu kizuri.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...