THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

Gadget

This content isn't available over encrypted connections yet.

HALMASHAURI YA MBINGA YAWASHAURI WANANCHI WAKE KUPIMA ARDHI

Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Mbinga mkoani Ruvuma Ambrose Mtarazaki akizungumza jana na wakazi wa kijiji cha Amani Makolo wakati wa zoezi la uhamasishaji wananchi kujiandaa kwa ajili ya mpango wa kupima ardhi ikiwemo mashamba hatua itayaosaidia wananchi kupata hati na kuzitumia kwa ajili ya kukopa fedha kutoka katika taasisi za fedha hapa nchini.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Mbinga mkoani Ruvuma Ambrose Mtarazaki akielekeza mpango wa upimaji ardhi jana kwa wakazi wa kata ya Maguu wilayani Mbinga ambapo halmashauri hiyo inakusudia kuanza kupima ardhi kuanzia viwanjia,nyumba za makzi na mashamba ili kuwafanya wamiliki wake kupata hati itakayotambulika kisheria.
Mkazi wa kijiji cha Amani Makolo kata ya Amani Makolo wilaya ya Mbinga Andrew Haule akiuliza swali wakati wa mkutano  uhamasishaji wa upimaji ardhi katika kijiji hicho ulioongozwa na mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Mbinga Ambrose Mtarazaki(hayupo pichani),Halmashauri ya wilaya ya Mbinga imeanza utaratibu wa kupima ardhi yote kwenye vijiji na miji midogo.
Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Mbinga Gombo Samandito, akizungumza jana na wakazi wa kata ya Maguu wilayani humo wakati wa zoezi la uhamasishaji wananchi kwa ajili ya kazi ya kupima ardhi itayofanywa na wataalam wa idara ya ardhi katika vijiji na miji midogo yote.Picha na Muhidin Amri.