Halmashauri ya wilaya ya Mufundi Mkoani Iringa imefanikiwa kutekeleza agizo la Waziri Mkuu wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania katika ukusanyaji wa mapato ya ndani, baada ya kukusanya zaidi ya Shilingi Bilioni 4.7 sawa na asilimia 82.7 kati ya bilioni 5.6 ilizopanga kukusanya katika mwaka wa Fedha 2015-2016.

Taarifa ya kitengo cha habari na mawasilino cha halmashauri ya Wilaya ya Mufindi, imetanabaisha kuwa, mafanikio hayo yamebainishwa na Mwenyekiti wa halmashauri ya Wilaya ya Mufindi Mh. FESTO MGINA kwenye kikao cha kawaida cha baraza la madiwani wa halmashauri hiyo kilichoketi mjini Mafinga.

MGINA amesema, mafanikio hayo ni matokeo ya ufuatiliaji na usimamizi mzuri wa vyanzo vya mapato vya halmashauri kama vile mapato yatokanayo na usafirishaji wa mbao na Magogo, kuuzwa kwa sehemu ya msitu wa halmashauri sanjari na ushuru unaokusanywa kwa wafanyabiashara wadogo katika halmashauri hiyo.

Aidha, Mwenyekiti huyo ameongeza kuwa, pamoja na kutekeleza agizo la Waziri Mkuu la kila halmashauri kukusanya mapato kwa asilimia 80 na kuendelea, kikwazo kikubwa cha kutofikia asilimia 100 ni kuzaliwa kwa halmashauri ya mji wa Mafinga jambo amabalo lilisababisha kugawana vyanzo vya mapato .

Mgina, ametaja mkakati wa kufidia vyanzo hivyo kwa mwaka mpya wa Fedha 2016-2017 kuwa ni pamoja na kuanzisha stendi katika miji midogo ya Igowole na Nyololo, kuimarisha doria nyakati za usiku kwa wafanyabishara wanaotumia njia za panya kusafirisha mbao na Magogo hususani nyakati za usiku sanjari na kuongeza vizuio katika vijiji.
Madiwani katika kikao cha baraza wakifuatilia kwa umakini.
Mkururugenzi mtendaji wa Halmashauri Dk. Riziki Shemdoe, akizungumza kama katibu wa kikao cha baraza.
Mwenyekiti wa halmashauri, Festo Mgina akizungumzia mafanikio ya ukusanyaji wa mapato.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Tumia sehemu ya mapato kuboresha huduma na mipango ya maendeleo ya kuinua hali ya maisha ya wakazi wote katika halmashauri yenu.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...