THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.


Gadget

This content isn't available over encrypted connections yet.

HIVI NI LINI HII MISHKAKI ITAFIKA TAMATI???

 Bodaboda zikiwa zimepakia abiria kwa mtindo wa Mshkaki huku wakiwa hawana kofia ngumu na hata wasiwasi pia ahawa. Upakiaji wa aina hii si salama kabisa kwa wasafiri hawa na inatakiwa ifike mahala huu utaratibu ufikie tamati, ili kuokoa maisha ya ndugu zetu hawa.


Kuna Maoni 3 mpaka sasa.

  1. Anonymous Anasema:

    Hii ni hatari mishikaki ikomeshwe bodaboda watoe ushirikiano kuimaliza

  2. HK Anasema:

    Hii 'Mishikaki' haitafikia tamati endapo vyombo husika hativakuwa 'serious' katika kukomesha jambo hilo. Nadhani kama kungekuwa na sheria kwa kila atakebainika na kukamatwa na huo Mshikaki wake, basi papo hapo atozwe faini kutegemea na hizo 'finyango' alizozidunga katika huo 'Mshikaki' wake (yaani kila kichwa), tena iwe faini kubwa kwa kila mmoja na kana kwamba haitoshi pia papo hapo taratibu na sheria zitowe adhabu ya kuizuwia leseni ya muhusika kwa muda wa miezi kadhaa na kuhakikisha hilo linafanyika kwa ufatiliaji wa karibu zaidi ili kuthibitisha linatekelezwa mara moja. Nadhani tukianza kwa adhabu kama hiyo, watatia akili na katu hawatoitamani tena hiyo 'Mishikaki' watakuwa radhi wale chips tupu (Wakose abiria) kuliko hiyo mishikaki inayohatarisha maisha na usalama wa abiria na kusababisha ajali za mara kwa mara.

  3. Anonymous Anasema:

    Huu ni kama mtego wa panya. Yo yote yule aweza kuumia au kupoteza maisha. Komesha yake ni rahisi kidogo.Kila mmoja katika mshikaki faini shillingi elfu kummi, na pikipiki ikamatwe kuwa mali ya serikali,simple, watakoma