Bodaboda zikiwa zimepakia abiria kwa mtindo wa Mshkaki huku wakiwa hawana kofia ngumu na hata wasiwasi pia ahawa. Upakiaji wa aina hii si salama kabisa kwa wasafiri hawa na inatakiwa ifike mahala huu utaratibu ufikie tamati, ili kuokoa maisha ya ndugu zetu hawa.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. Hii ni hatari mishikaki ikomeshwe bodaboda watoe ushirikiano kuimaliza

    ReplyDelete
  2. Hii 'Mishikaki' haitafikia tamati endapo vyombo husika hativakuwa 'serious' katika kukomesha jambo hilo. Nadhani kama kungekuwa na sheria kwa kila atakebainika na kukamatwa na huo Mshikaki wake, basi papo hapo atozwe faini kutegemea na hizo 'finyango' alizozidunga katika huo 'Mshikaki' wake (yaani kila kichwa), tena iwe faini kubwa kwa kila mmoja na kana kwamba haitoshi pia papo hapo taratibu na sheria zitowe adhabu ya kuizuwia leseni ya muhusika kwa muda wa miezi kadhaa na kuhakikisha hilo linafanyika kwa ufatiliaji wa karibu zaidi ili kuthibitisha linatekelezwa mara moja. Nadhani tukianza kwa adhabu kama hiyo, watatia akili na katu hawatoitamani tena hiyo 'Mishikaki' watakuwa radhi wale chips tupu (Wakose abiria) kuliko hiyo mishikaki inayohatarisha maisha na usalama wa abiria na kusababisha ajali za mara kwa mara.

    ReplyDelete
  3. Huu ni kama mtego wa panya. Yo yote yule aweza kuumia au kupoteza maisha. Komesha yake ni rahisi kidogo.Kila mmoja katika mshikaki faini shillingi elfu kummi, na pikipiki ikamatwe kuwa mali ya serikali,simple, watakoma

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...