Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Hatari,Kazi ipo. Kwa kweli biashara yeyote lazima ikue na faida yake ionekane au la sivyo ifeli na ife kwa kushindwa kujizalisha. Lakini ukiona biashara ipo ipo tu haikui wala haifi moja kwa moja basi ujue kuna namna hapo. Kinachokera kwa nchi yetu hakuna hata shirika au biashara ya umma iliyoanzishwa na kujizalisha maradufu na kujiendesha yenyewe na kujipanua zaidi na kuzalisha vitega uchumi vyengine. Mfano mzuri vipi shirika la ndege li feli wakati kuna mahitaji ya usafiri hali ya juu? Ndege moja kubwa kama itafanya kazi bila ya kupata matatizo kwa kipindi kifupi lazima inunue ndege nyengine. Lakini kwa kwetu Tanzania kila kitu kinachoanzishwa cha umma lazima kidumae. Simba na yanga ni mifano halisi ya jinsi gani taasisi za umma Tanzania zinavyoendeshwa. Tanzania ni tajiri kama zilivyo simba na yanga lakini watu wachache ndio wanaojinufaisha kwa kuendekeza ubinafsi. Vipi nchi yenye vivutuo vya utalii vya kila aina inakosa shirika la ndege la Maana? Umasikini mwengine ni wa kujitakia. Maghufuli katumia uzalendo na ari zaidi ya kununua ndege kwa pesa Cash ni jambo nzuri kwani mashirika ya wenzetu ya wazungu kitendo kama hicho ni kujijijengea sifa nzuri ya kiuminifu katika biashara na hasa katika kujisafishia mazingira ya mikopo. Lakini kwa utajiri tulionao Tanzania tunauwezo wa kukopa ndege kubwa za kibiashara na kuhakikisha shirika husika linafanya kazi kwa faida na kujilipia gharama lakini kwa hali ilivokuwa nchini ilifikia pabaya ni vigumu kulichukulia dhamana shirika lolote la umma ni kitendo cha kuingiza nchi kwenye mzigo wa madeni zaidi, na kwa wale wote wanaoitakia mema Tanzania lazima wamuunge mkono muheshimiwa Maghufuli kwani vita anayopigana ya ufisadi ni nzito mno na kulegeza kumuunga mkono kwa dhati ni kuwapa nguvu mafisadi na waovu wote wa maendeleo ya nchi yetu.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...