Kocha  Mkuu  wa timu ya mpira wa miguu wa ufukweni (Beach Soccer), John Mwansasu akizungumza na waandishi wa Habari jijini Dar es Salaam leo. Kushoto ni Afisa Habari wa Shirikisho la Mpira wa Miguu(TFF), Alfred Lucas.

Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.
KOCHA Mkuu  wa timu ya mpira wa miguu wa ufukweni (Beach Soccer), John Mwansasu, ametangaza kikosi cha wachezaji 16 watakaoingia kambini kwa ajili ya kujiandaa na mchezo wa Mpira wa Miguu wa Ufukweni utakaofanyika Agosti 26, mwaka huu dhidi ya Ivory Coast wa kuwania nafasi ya kucheza fainali za Kombe la Mataifa Afrika.

 Mchezo huo utachezeshwa na waamuzi kutoka Uganda ambao ni Shafic Mugerwa katikati na wasaidizi wake ni Ivan Bayige Kintu na Muhammad Ssenteza, mwamuzi wa mezani atakuwa Adit Ouchker wa Morocco huku Kamishna akiwa ni Reverien Ndikuriyo wa Burundi. 

Timu hizo zinatarajiwa kucheza mechi mbili ambapo mara baada ya mchezo wa Dar es Salaam, utarudiwa mwingine huko Ivory Coast na mshindi wa jumla atakuwa amefanikiwa kufuzu kwa fainali.

Akizungumza na wandishi wa habari Mwansasu amesema kikosi hicho kinaundwa na wachezaji sita kutoka Zanzibar na 10 Tanzania Bara na  wanatarajiwa kucheza mechi mbili ambako mara baada ya mchezo wa Dar es Salaam, watarudiana huko Ivory Coast na mshindi wa jumla atakuwa amefanikiwa kufuzu kwa fainali.

Kikosi hicho kinaunda  na wachezaji Talib Ame,  Ahamada,  Mohammed Makame, Ahamed Rajab (golikipa) Khamis Said na Yacob Mohamed wote kutoka Zanzibar.

Wengine ni Ally Raby, Mwalimu Akida, Khalifa Mgaya, Rolland Revocatus, Juma Sultan, Rajab Ghana, Samwel Salonge, Kashiru Salum, Juma Juma na Kevin Baraka.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...