1. Brunei ukipenda iite 'Darusalaam' ama nyumba ya amani ni nchi ambayo raia wake hawalipi kodi yeyote (All citizens in Brunei, including expats, do not have to pay for taxes, for it is absolutely free.), Hata maisha ya wananchi wake ni mazuri na mshahara wa chini kabisa ni dola 25 kwa saa (Tshs 50,000) huku ukosefu wa ajira ukiwa ni wastani wa 5% tu. Serikali inalipa gharama zote muhimu, mpaka chakula kinalipiwa ruzuku. ukifanya kazi kule hakuna income tax (There is no personal income tax or capital gains tax). Sultani anasimamia vizuri sana export ya mafuta na gesi na wanachi wanakula bata watakavyo.

GDP ya Brunei imepanda hadi 56% kuwa nchi ya tano duniani (16.11 billion USD in 2013) na IMF wanasema nchi hiyo haidaiwi HATA MIA....
2. Sultan wa Brunei Mohammad Hassan Bolkiah ndiye Raisi tajiri kuliko maraisi wote duniani, Maarufu kwa utumiaji wa dhahabu kwa kila kitu, hali ila na vijiko vya dhahabu, na nguo anazo vaa zimepambwa kwa dhahabu na fedha. Huyu anamiliki Jumla ya MAGARI 5000 YA KIFAHARI (tazama kasri na moja ya gari lake lake la dhahabu tupu pichani).

Sultan huyu anamiliki pia ndege aina ya Boing 747 thamani yake ikiwa ni dola milion 100 ambamo pia nakshi pekee ni dola milioni 120 humo utakuta vyoo na vyumba vya dhahabu, pia anamiliki ndege ndogo sita na helicopta moja. Arusi ya mtoto wa Sultan wa Brunei ilifanyika kwa muda wa siku 14 kwa gharama ya 5 milion dolla huku watu wote walioalikwa wakila na kunywa na kusaza, na kuhudhuriwa na zaidi ya maraisi 25.
3. Elimu ni Bure kabisa na watoto chini ya miaka 12 HUTIBIWA BURE huku watu wazima wakilipia dola 1 tu kwa Matibabu. Kadhalika ukioa tu unapewa na gari. Ni nchi mojawapo ambayo ina uwiano mkubwa wa watu na magari (1:209)-Ikiwa hakuna tiba ya ugonjwa wako Brunei unapelekwa nje ya nchi hasa Malaysia na Singapore kwa gharama za serikali

4. Pombe imepigwa marufuku kabisa kisiwani Brunei ingawa wageni wanaweza kuagiza kiwango chenye ukomo na Hakuna NOA/NGURUWE hata mmoja nchi nzima....................

5. . Ukiwa Brunei marufuku kupoint kutumia kidole cha shahada kuonesha kitu. Kidole gumba tu hutumika kupoint kitu na ni Lazima kuvua viatu unapoingia nyumba yeyote ndani ya Brunei

6. Hii inatumia mfumo wa SHARIA ambapo 'Wezi hukatwa mikono na wazinifu kupigwa mawe'. Mwaka 2014 ilipitisha sheria ya kupigwa kwa mawe hadi kufa yeyote atakayebainika anafanya USHOGA (Homosexual) lakini kwa uthibitisho wa mashahidi WANNE.....Unaweza kusherehekea Noeli (X-mass) lakini si kwa kuweka mapambo yake kama vilemti wa Xmass nk..........

7. Ingawa Kisiwa cha Brunei Kina BUNGE lakini nchi hiyo HAINA UCHAGUZI......Uchaguzi wa mwisho ulifanyika mwaka 1962, kuna chombo kimoja tu cha habari kinachomilikiwa na Serikali...ni aghalabu sana kwa media kuipinga serikali

8. 93% YA WATU WOTE WAMEENDA SHULE KWA KIWANGO CHA LAMI (Degree)

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. Inafurahisha sana ustaarabu wao. Nchi ina natural resources, na faida yake inatumika kwa wananchi ambao ni mali yao waliyopewa na Subhana. Inafurahisha pia kuondoka kwa janga la pombe,pombe inatutia doa sana kwenye maisha yetu, lakini mtu hasubutu kuipinga kwani wauza/watengenezaji wa pombe wana mabavu. Mungu awazidishie na Mungu atusaidie nasi tuendelee.

    ReplyDelete
  2. Hizi simulizi zinafanya wadada wasisome kwa bidii wakidhani wataolewa na mwanamflme wawe na wakuwafanyia kazi. Mwishoe wajikuta wao ndo wafyekaji

    ReplyDelete
  3. Hawa wana watu wachache karibu laki tano na raslimali nyingi. Sasa sisi watu milioni arobaini na tano, kipato siyo kikubwa, nchi kubwa, mahitaji ya kuboresha miundo mbinu na huduma za maji, barabara, nishati, makazi bora na biashara yapo. Serikali kwa sasa hivi inahitaji kodi ili iweze kutoa huduma, kulipa mishahara na kulipia madeni Sekta binafsi itabidi ikue kwa haraka na ile 0isiyo rasmi irasimishwe iili kuongeza watanzania wenye kipato cha kuchangia kodi ikiwemo ile ya kutokana na matumizi ya kila siku.

    ReplyDelete
  4. Duh sasa hawa wakimbizi wanaozuiwa na wengine kukataliwa si ndio ingekua poa sana pande hizo au wamestukia kua si lolote huko Brunei zaidi ya stori tu. Mwandishi habari yako imesheheni mafuta mpaka raha....ninachojiuliza ni kwamba sisikii watu wakitamani kwenda huko au wanaogopa kupigwa mawe na kukatwa viganja. NOA...hahahahhaha

    ReplyDelete
  5. Yes, mbona hamuelezi GDP ni ngapi. Resources nyingi watu wachache. Hili ni muhimu kuliweka wazi pia. Watanzania wasidhani ni kwa sababu wao serikali zao zimekuwa hazifanyi chochote.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...