Na Geofrey Chambua

VATICAN ni nchi yaliko makao makuu ya Kanisa Katoliki.

Nchi hii ina mambo mengi ambayo yapo tofauti na nchi nyingine duniani. Baadhi ya mambo machache ni haya yafuatayo:

VATICAN CITY
VATICAN ni nchi yaliko makao makuu ya Kanisa Katoliki.
Nchi hii ina mambo mengi ambayo yapo tofauti na nchi nyingine duniani. Baadhi ya mambo machache ni haya yafuatayo:
1. Ndio nchi ndogo kuliko zote duniani ikiwa na ukubwa wa 44 hectare(110 acres). Ikiwa na jumla ya watu 800 kwa mujibu wa data za hivi karibuni (2014) na hadi kufikia mwaka 2011, nchi nzima ilikua na WANAWAKE 32 tu na wote wanajulikana kazi zao na wanapoishi ( According to the Herald Sun, there were "only 32 female citizens" residing by 2011) . Karibu nusu ya Raia wake wanaishi nje ya nchi wakiwemo mabalozi waliotapakaa karibu kote duniani ingawa Mabalozi wa nchi za Kigeni kwa Vatican huishi katika Jiji la Roma

2. Ilikuwa nchi kamili Feb 11, 1929 baada ya Benitto Mussolini(kwa niaba ya Mfalme wa Italy) kutiliana saini na Pietro Gasparri(kwa niaba ya Pope) hivyo kuwa nchi huru ndani ya jiji la Roma.

3. Kiongozi wa nchi hii (Pope) ndie kiongozi pekee anaeongoza nchi kifalme baada kuchaguliwa kwa kupigiwa kura. Papa aliwahi kuishi miaka 60 ndani ya Vatican bila KUSAFIRI NJE ya nchi. Askari wote wanaomlinda Pope wana asili ya Uswis,na hujulikana kama Swiss Guard
4. Ni nchi pekee yenye waumini wa dini moja huku 99% kati yao wakiwa ni wasomi wa elimu ya juu na 75% ya Raia wake wamepitia mafunzo ya kishushushu. Ni moja ya nchi zenye Intelejensia ya hali ya juu sana duniani

5. Inasemekana kanisa la St.Peter yalipo makao ya Papa huwa linaongezeka ukubwa kutokana na wingi wa watu,Ni sehemu pekee ambapo karibu la Mtume Petro linapatikana (St Peter's Basilika)

6. Benki ya Vatikani ambayo pia hujulikana kwa jina la Institute for Works of Religion inafanya shughuli za kibenki duniani kote ambayo ATM zake zina maelekezo kwa Kilatini tu.
7. Ni nchi pekee duniani isiyokuwa na mapato yatokanayo na kodi. vyanzo vikuu vya mapato ni mauzo ya stempu na viingilio kwenye majumba ya kale toka kwa watalii................kadhalika wafanyakazi wote ndani ya Vatican hawatozwi kodi yoyote

8. Ni mojawapo ya nchi mbili duniani ambazo hazina sheria ya TALAKA, nyingine ni Filipine. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...