Katika siku za hivi karibuni, kumekuwepo na
mitazamo tofauti miongoni mwa jamii kufuatia kuonekana kwa askari polisi wakifanya
mazoezi katika maeneo mbalimbali hapa nchini.
Kufuatia hali hiyo, jeshi la polisi nchini, linatumia
fursa hii kuwatoa hofu wananchi kwamba mazoezi hayo ni ya kawaida kwa askari wa
jeshi la polisi.
Aidha, jeshi la polisi linawataka wananchi kuendelea
na shughuli zao za kawaida kwa sababu mazoezi hayo hayalengi kuzuia shughuli
zozote halali zinazofanywa na wananchi.
Imetolewa
na:
Advera John Bulimba - Kamishina Msaidizi wa Polisi
(ACP)
Msemaji wa Jeshi la Polisi,
Makao Makuu ya Polisi.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...