Rais Mstaafu Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akiweka udongo kwenye kaburi la Bi Shakila Said,wakati wa maziko huko nyumbani kwake Mbagala Charambe,jijini Dar es salaam leo Agosti 20, 2016.
Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mh.Nape Nnauye akiweka udongo kwenye kaburi la Bi Shakila Said,wakati wa maziko huko nyumbani kwake Mbagala Charambe,jijini Dar.
Rais Mstaafu awamu ya nne,Dkt Jakaya Kikwete akiweka saini kitabu cha maombolezo cha Bi Shakila Said ,huko nyumbani kwake Mbagala Charambe,jijini Dar,wa pili kushoto aakishuhudia ni Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mh.Nape Nnauye na Katibu wa Shirikisho la Muziki Tanzania Bw. John Kitime.
Makamu wa Rais Mama Samia Suluhu Hassan akiweka saini kitabu cha maombolezo cha Bi Shakila Mbagala Charambe,jijini Dar es salaam. Kushoto ni  Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mh.Nape Nnauye.
 Mke wa Rais Mstaafu Mama Salma Kikwete akiweka saini kitabu cha maombolezo cha Bi Shakila Said  huko nyumbani kwa marehemu  Mbagala Charambe,jijini Dar es salaam.
Rais Mstaafu awamu ya nne,Dkt Jakaya Kikwete (wa pili kulia) na Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mh.Nape Nnauye (pili kushoto) wakishiriki maziko ya aliyekuwa Mkongwe,mwimbaji mahiri wa muziki wa Taarabu hapa nchini,Bi Shakila Saidi ambaye mazishi yake yamefanyika leo huko nyumbani kwake Mbagala Charambe,jijini Dar.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Hakika "Kullu Nafsi Dhaiqatul Mawt'
    Mola akughufirie kwa yote, akunusuru na adhabuze zote, kupe kauli thabit, akujaaliye safari ya kheri na In Sha Allah kesho 'Yaumul Hisabu' ukawe miongoni mwa waja wake wema watakaoingia katika yake 'Jannatu Nnaeem'. Pumzika pema Peponi Mama yetu, kipenzi chetu, ndugu yetu Bi Shakila Bint Saidi. AMEN.

    ReplyDelete
  2. Poleni wafiwa. Mola awape wepesi katika kipindi hiki kigumu.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...