Jumuiya ya watanzania waliosoma China – CAAT wameishauri serikali kuwatumia wasomi hao katika kuhakikisha inanufaika na mikataba na masuala mbalimbali yahusuyo TANZANIA na CHINA. 


Wakizungumza katika mkutano mkuu wa kuchagua uongozi mpya wa jumuiya hiyo wanachama wa CAAT wameeleza kuwa Watanzania waliosoma China wanaijua nchi hiyo vizuri, tabia za wachina na lugha yao hivyo wakishirikishwa kabla ya kusainiwa kwa mikataba au kuingia makubaliano yeyote wanaweza kuwa chachu ya nchi kunufaika zaidi.

Mwenyekiti wa kwanza wa jumuiya hiyo Dk.Mhame Paulo aliyeenda kusoma china miaka ya 80 amesema, sera ya Tanzania ya viwanda inaweza kutimia ndani ya miaka mitano kwakuwa Tanzania inauwezo wa kuzalisha na kuuza katika soko la China akitolea mfano uwezo wa Tanzania kutengeneza dawa za kutibu ugonjwa na pumu na kuziuza katika soko la China na dunia kwa ujumla.

Mwenyekiti mpya wa CAAT, Dk.Liggyle Vumilia akishukuru baada ya kuchaguliwa amesema wanachama wa jumuiya hiyo wakitumika Tanzania itapata manufaa kwakuwa wanachama wake wanajua kuongea kichina, wanajua tabia za wachina na wanaielewa china vyema kiasi cha kujua kitu gani kinapatikana wapi hivyo serikali ikiwatumia itaepuka udanganyifu unaofanywa na baadhi ya watu wasiokuwa wazalendo.

Uchaguzi wa jumuiya wa watanzania waliosoma China umewaweka madarakani viongozi wa masuala mbalimbali ikiwemo Mwenyekiti, katibu, mwekahazina, mkurugenzi wa masuala ya bisahara na uwekezaji, mkurugenzi wa sanaa, utamaduni na utalii, mkurugenzi wa masuala ya elimu na Tehama pamoja na mkurugenzi wa takwimu , habari na mawasiliano.

Uhusiano wa Tanzania na China una zaidi ya miaka hamsini na watanzania wamenufaika na uhusiano huo katika nyanja mbalimbali ikiwemo kwenda kusoma china na idadi yao kuzidi kuongezeka kila mwaka hali iliyopelekea kuundwa jumuiya watanzania waliosoma China. Tayari jumuiya hiyo ya watanzania waliosoma China imekwishapata usajili katika wizara ya mambo ya ndani ya nchi tangu mwezi wa Juni 2016.

mwenyekiti aliyemaliza muda wake Dk. Mahame Paulo akizungumza na wanajumuiya ya CAAT
Wanachama wa CAAT wakiwasikiliza viongozi wao wa mpito
Gustavu Sanga Gustavu Sanga mwenyekiti wa uchaguzi CAAT akitoa maelekezo kwa wajumbe wa CAAT

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...