THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

Gadget

This content isn't available over encrypted connections yet.

JWTZ BINGWA WA MPIRA WA PETE MICHUANO YA MAJESHI NCHI ZA AFRIKA MASHARIKI

Na Selemani Semunyu JWTZ
Timu ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania JWTZ kwa Mpira wa Pete wametangaza ubingwa wa michuano ya majeshi kwa Nchi za Afrika mashariki kwa mchezo huo yanayoendelea katika Uwanja wa Amahoro Kigali Nchini Rwanda.,
Tanzani]a ilifikia hatua hiyo baada ya kuifunga timu ya Kenya  39-33 katika Mchezo uliokuwa vuta nikuvute ikiwa ni mchezo wa tatu mfululizo kwa Timu hiyo kushinda na hivyo kupata alama ambazo haziwezi kufikia na Timu yeyote.
Katika Mchezo huo Tanzania ilianza vyema tangu Robo ya Kwanza ambapo ilitoka 17-13 wakati robo ya pili 20-16 huku robo ya Tatu wakitoka 31 kwa 24 na mwisho Tanzania kuibuka Washindi.
Nahodha wa Tanzania Dorita Mbunda alisema wanafuraha kwa kurejesha ubingwa walioupoteza mwaka jana na kuchukuliwa na Uganda.
Nahodha wa Uganda Carlo Alepo alisema walikuwa na wachezaji wachanga amabao ni wageni katika mashindano hivyo wanajiandaa kwa michuano ijayo kwani wachezaji wao watakuwa na uzoefu Tayari wa Mashindano.
Kikosi cha Tanzania kilichoibuka na Ushindi huo  ambacho kilicheza Mwanzo had Mwisho wa mchezo huo ni  Dorita Mbunda,Faraja Malaki,Joyce Kaira,Veronica Patric,Mwanaidi Hassan,Nasra Suleiman Na Lulu Joseph.
Kwa upande wake  MaKocha wa Timu hiyo Grace Mgyabuso na Argentina Kienzevya kwa Nyakati tofauti walisema  ahadi waliyoitoa kwa Watanzania na Mkuu wa majeshi wameitimiza kilichobaki ni kusubiri kukabidhiwa kombe.
Naye Kanali  Mary Hiki wa Tanzania  aliwapongeza wachezaji na kuwashukuru Watanzania kwa maombi yao yaliyowawezesha kuibuka na ushindi huo ambao aliuita ni muhimu kwa Taifa.
Awali Timu ya Tanzania iliifunga Timu ya Rwanda ambayo ni mabingwa wattezi kabla ya Kuwafunga Wenyeji Rwanda kwa matokeo ambayo hayajafikiwa na Timu yeyote katika Michuano hii.
 Mchezaji wa kati wa Timu ya Pete ya Tanzania (C) Faraja Malaki akiwa katika heka heka za mchezo wakati wakikabiliana na Timu ya Kenya  Katika Uwanja wa Amahoro Kigali Rwanda ambapo  Tanzania ilishinda 39-33(Picha Na Dora Mushi) .
 Mchezaji  Mpira wa Mikono wa  Tanzania Bonnerge Kasanga (mwenye Mpira) akiwa katika heka heka za mchezo wakati wakikabiliana na Timu ya Kenya  Katika Uwanja wa Amahoro Kigali Rwanda ambapo  Tanzania ilifungwa 26-15
 Mchezaji wa wa Timu ya Pete ya Tanzania (GA) Nasra Suleiman  akiwa katika heka heka za mchezo wakati wakikabiliana na Timu ya Kenya  Katika Uwanja wa Amahoro Kigali Rwanda ambapo  Tanzania ilishinda 39-33
 Kiongozi wa msafara wa Timu za Tanzania Brigedia Jenerali Jairosi Mwaseba akisalimiana na majeshi kwa Nchi za Aachezaji wa Timu ya mpira wa Kikapu ya Tanzania katika uwanjani  wa Ndani wa Amahoro Kigali Rwanda wakati wa mashindano ya Ahariki kwa majeshi 
 Timu ya Pete ya Tanzania  katika Picha ya pamoja kabla ya kuanza kwa Mchezo wake  Dhidi ya Kenya  Katika Uwanja wa Amahoro Kigali Rwanda ambapo  Tanzania ilishinda 39-33
Picha zote na  Dora Mushi.