Aliyekuwa
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa na ambaye sasa ni
Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Usalama wa Taifa Dr. Modestus Kipilimba leo
amekabidhi rasmi ofisi kwa Kaimu Mkurugenzi Mkuu mpya Bw. Andrew Wilson
Massawe; aliyeteuliwa hivi karibu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuwa
Kaimu Mkurugenzi Mkuu NIDA.
Katika
Hafla fupi ya makabidhiano iliyofanyika Makao Makuu ya Mamlaka ya Vitambulisho
vya Taifa NIDA, Dr. Modestus Kipilimba amekabidhi ripoti yenye mjumuisho wa
taarifa ya utekelezaji mradi wa Vitambulisho vya Taifa na hatua za utekelezaji.
Halfa
hiyo ilifuatiwa na ziara fupi ya kutembelea kituo cha uchakataji taarifa na
uzalishaji vitambulisho (Data Centre) ambapo mbali na kukagua shughuli za
uzalishaji, Bw. Massawe alipata fursa ya kukagua mitambo na ubora wa
vitambulisho vinavyozalishwa.
Dr.
Modestus Kipilimba (Kushoto) akimkabidhi ripoti ya utekelezaji mradi wa
vitambulisho vya Taifa Bw. Andrew Wilson Massawe aliyeteuliwa kuwa Kaimu
Mkurugenzi Mkuu NIDA wakati wa hafla ya Makabidhiano katika ofisi za Makao makuu ya NIDA jijini Dar es salaam.
Kaimu
Mkurugenzi Mkuu NIDA, Bw. Andrew Wilson Massawe akizungumza na wajumbe wa
Menejimenti ya Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa mara baada ya hafla ya
makabidhiano
Kaimu
Mkurugenzi Mkuu NIDA, Bw. Andrew Wilson Massawe akikagua mitambo ya uzalishaji
vitambulisho alipotembea kituo cha uchakataji na uzalishaji vitambulisho mara
baada ya halfa ya makabidhiano. Kulia ni Dr. Modestus Kipilimba
Kaimu Mkurugenzi Mkuu NIDA, akikagua mfumo wa
uhifadhi taarifa wakati alipotembelea kituo cha uchakataji taarifa (Data
Centre) na kushuhudia mfumo wa kielektroniki unavyoendesha shughuli
mbalimbali za uzalishaji na uhifadhi wa taarifa katika kituo hicho
Dr. Modestus Kipilimba (kushoto) na
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa NIDA Bw. Andrew Wilson Massawe wakiwa katika picha ya pamoja na Menejimenti ya NIDA, baada
ya hafla fupi ya makabidhiano
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...