Kaimu Mkurugenzi Idara ya Utamaduni, Lily Beleko kutoka Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo akizungumza jambo kabla ya Uzinduzi wa Kitabu cha Ukristo katika Ukumbi wa Baraza la Maaskofu Dar es Salaam
 Mkurugenzi wa Mkuki na Nyota Publishers, Walter Bgoya akizungumza jambo kabla ya uzinduzi wa kitabu cha Ukristo
 Katibu Mtendaji Baraza la Kiswahili  la Taifa (BAKITA), Dk. Selemani Sewangi akionesha kitabu hicho kwa wadau na kwa waandishi wa habari wakati wa hafla fupi ya Uzinduzi huo wa kitabu cha Kamusi ya Ukristo kilicho zinduliwa na  Kaimu Mkurugenzi Idara ya Utamaduni, Lily Beleko kutoka Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo.
 Kaimu Mkurugenzi Idara ya Utamaduni, Lily Beleko (katikati) kutoka Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo akizindua Kitabu cha Kamusi ya Ukristo katika hafla iliyofanyika Jijini Dar es Salaam. kulia ni Mhadhiri Chuo Kikuu Katoliki (WEA) Nairobi na Mhariri Mkuu wa Kampuni ya Uchapishaji ya Gaba Publications , Padri, Dk.Jordan Nyenyembe  ambaye ndie mtunzi wa kitabu hicho na Padri Ubaldus Kidavuri  
(PICHA ZOTE NA KHAMISI MUSSA)

SERIKALI inawashauri viongozi wa dini nchini  kuendelea kutafsiri maneno magumu ya kidini  ili kuepusha chuki, vurugu, ghasia na mapigano  katika jamii.
Kauli hiyo ya  Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo ililisomwa na Kaimu Mkurungezi wa Maendeleo ya Utamaduni, Lilly Beleko katika uzinduzi wa ‘Kamusi ya Ukristo’ jijini Dar es Salaam .
Alisema kuzinduliwa kwa kamusi itahamasisha na kurahisisha uelewa wa vitabu na maandiko kwa usahihi na ufasaha kwa jamii na kuleta upendo, Utulivu na Amani.
“Lugha yetu ya Kiswahili ni chombo muhimu cha mawasiliano ambachokimekuwa kiungo cha kuimarisha umoja, Amani na uzalendo, hivyo lazima tukiendeleze,” alisema.
Alisema serikali itaendelea kuunga mkono juhudi za  za kukuza na kuendeleza lugha ya Kiswahili na kuthamini  wanataaluma na wadau wa harakati za kutetea hadhi ya Kiswahili.
Mwakilishi wa Katibu Mkuu wa Baraza la Maaskofu Tanzania (TEC) Padre Abadius Kidavule alisema ni mara ya kwanza Tanzania ndani ya Kanisa Katoliki kuzinduliwa Kamusi ya Ukristo.
“Ni jambo la  kujivuni  kuzindua kamusi, hivyo watanzania wanapaswa kukinunua ili wajisomee,” alisema.
Mwandishi wa Kanusi hiyo, Dk.Jordani N Yenyembe alisema watanzania tumefanya makosa kutopenda kusoma vitatu, hali imesabisha kupatikana waandishi wachache wa vitatu.
“Wengi hawapendi kukosomewa  na wakikosolewa kutokana na uandishi wao, hususa kuandika  mimi naendelea kuandika nahitaji kukolewa kwenye kamusi hii,” alisema

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Itabidi na dini nyengine wato kamusi yao ili tujue ukiongea na dini ipi utumie neno lipi.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...