Jumla ya watoto 49 wameonwa na madaktari bingwa kutoka taasisi ya Mifupa, Ubongo na mishipa ya fahamu Muhimbili, wanaozunguka nchi nzima kutibu watoto waliozaliwa kwa tatizo la vichwa vikubwa na mgongo wazi, katika kambi tiba inayodhaminiwa na GSM Foundation katika harakati za kuokoa maisha ya watoto hao, tatizo ambalo linasadikika kupoteza maisha ya watoto wengi zaidi nchini.

Kwa mujibu wa Kaimu kiongozi wa Kambi tiba hiyo ambayo leo imemaliza shughuli zake mkoani Ruvuma na sasa inaelekea Mkoani Mbeya, Dk Hamisi Shabani, kati ya watoto 49 walioingia maabara, ni wattoto 12 tu walioweza kufanyiwa upasuaji na hii inatokana na hali za kiafya walizokutwa nazo watoto hao.

Wataalam wanaoshiriki kambi tiba kutoka MOI na GSM Foundation wakiangalia picha za CT Scan kabla ya kuanza tiba mkoani Ruvuma.

Utafiti uliofanywa na Taasisi ya MOI mwaka 2002, jumla ya watoto 4800 huzaliwa kila mwaka wakiwa na vichwa vikubwa na mgongo wazi, lakini kati yao ni watoto 500 tu ndio wanaoweza kufika hospitalini na kupata tiba huku changamoto kubwa ikiwa ni hali ya kiuchumi na imani za kishirikina.

Utafiti unaeleza kwamba wazazi wengi wanaozaa watoto wenye vichwa vikubwa, huwaficha ndani au kuwapeleka kwa waganga wa kienyeji wakiamini kwamba tatizo hilo ni la kishirikina,

Kiuhalisia, Tanzania ina madaktari bingwa 7 tu wenye uwezo wa kutibu watoto wanaozaliwa na vichwa vikubwa na mgongo wazi, kati yao, sita wanafanya kazi Muhimbili Dar es Salaam, na mmoja anafanya kazi katika Hospitali ya rufaa ya Bugando, jijini Mwanza.

Kambi tiba ya GSM inayojumuisha madaktari wanne, manesi wanne na mabwana usingizi wawili kutoka Taasisi ya Mifupa na Upasuaji ya Muhimbili Dar es Salaam.
Dk Mwanaabasi (Aliyeshika Daftari) akimruhusu Mmoja kati ya watoto waliofanyiwa upasuaji Tausi Kambona baada kuonekana kama anaendelea vizuri.
Dk John Mtei akimuangalia mtoto Mariam Juma Said, ambaye alifanyiwa upasuaji baada ya jopo kujiridhisha kwamba yuko tayari kwa tiba.
Maandalizi ya upasuaji yakiendelea katika maabara ya Hospitali kuu ya mkoa wa Rvuma.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...