Kambi tiba inayoendeshwa na Taasisi ya Mifupa na upasuaji ya Muhimbili kwa ufadhili wa GSM Foundation inayojaribu kuokoa maisha ya watoto wanaozaliwa na vichwa vikubwa na mgongo wazi leo imeanza kazi Mkoani Iringa, ukiwa ni mkoa wa nne tangu msimu wa pili wa ziara yake ya kuzunguka nchi nzima kuanza.

Kaimu mkuu wa kambi tioba hiyo, Daktari Bingwa Hamis Shaaban kutoka MOI amesema kwamba kumekuwa na hamasa ndogo kwa wazazi kuleta watoto wao kwa ajili ya tiba hii ya bure katika msimu huu, ukilinganisha na msimu wa kwanza ambapo jumla ya watoto 101 walifanyiwa upasuaji,



Katika awamu hii ya pili, mpaka leo hii ni watoto 35 wamefanyiwa, huku ukiwa ni mkoa wa mwisho kwa kambi hii kupita, hali inayoleta ukweli kwamba inaweza kumalizika bila kufikia lengo la kutibu watoto 100 na zaidi kama ilivyokuwa awamu ya kwanza.

Afisa habari wa GSM Foundation, Bw Khalphan Kiwamba, `Kiwadinho', amesema sababu kuu ni wagonjwa kuwa mbali na eneo ambapo tiba inafanyika, na kambi haikuweza kusogea zaidi kwa sababu za kiufundi kwani upasuaji wa watoto hawa unahitaji maabara za kisasa ambazo zinapatikana katika Hospitali za mikoa tu.

Kiwamba kwa upande wake amewaomba wakazi wa iringa kujitahidi kupashana habari ili watoto wengi wapate kupata tiba hii iliyofadhiliwa tayari,

Kambi tiba ya GSM kwa msimu huu wa pili inamalizika Agosti 18 mwaka huu wa 2016, ambapo baada ya tathmini, tarehe za msimu wa tatu zitatangazwa.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Ongeza matangazo ikiwemo radio na kushirikisha uongozi wa vijiji ili huduma hii iwafikie wenye mahitaji ili wapate huduma hii.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...