THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

Gadget

This content isn't available over encrypted connections yet.

KAMISHNA JENERALI WA JESHI LA ZIMAMOTO NA UOKOAJI ATEMBELEA SHIRIKA LA TAIFA LA UTANGAZAJI (TBC)Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Thobias Andengenye afanya ziara Shirika la Taifa la Utangazaji (TBC) kwa kumtembelea Mkurugenzi Mkuu wa Shirika hilo Dk. Ayoub Rioba ili kujifunza na kukuza mahusiano kati ya Taasisi hiyo na Jeshi hilo.
Katika ziara hiyo Kamisha Jenerali, alitembelea ofisi za Shirika hilo zilizopo Mikocheni jijini Dar es salaam, mapema leo asubuhi na  alipata fursa ya kujifunza jinsi gani shirika hilo linavyoendesha shughuli zake pamoja na kuwa na mazungumzo ya kina na mkurugenzi huyo. “Nimejifunza mengi lakini pia nashukuru kwa kupata fursa ya kutembelea na kuona ni jinsi gani tunaweza kushirikiana na shirika hili ili tuweze kuelimisha umma” alisema Kamishna Jenerali.
Akiwasilisha taarifa ya uendeshaji wa Jeshi hilo Kamishna Jenerali alimueleza changamoto zinazolikabili Jeshi hilo na nia ya yeye kutembelea ofisi hiyo ni kudumisha mahusiano ambayo yatakuwa chachu kwa taasisi hizo kwa manufaa ya umma.
Mkurugenzi wa shirika hilo naye alisisitiza kuwa nivema sasa Jeshi hilo likashirikiana na Shirika hilo ili kutekeleza dhima ya kuokoa maisha na mali, kwa kutumia chombo hicho pamoja na kuwa bajeti ya serikali ni finyu. “Kituo chetu ni cha umma na kwakuwa kazi zetu ni kuisaidia umma wa watanzania tupo tayari kushirikiana”, alisema Mkurugenzi mkuu wa TBC.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Taifa la Utangazaji (TBC) Dk. Ayoub Rioba akimkabizi kitabu ta wageni Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Thobias Andengenye alipotembelea ofisi za Shirika hilo mikocheni mapema leo asubuhi. 
 Mkurugenzi wa Matukio wa Shirika la Taifa la Utangazaji (TBC) Bi Martha Swai (wa kwanza kulia) akitoa maelezo jinsi ya upokeaji wa habari za matukio mbalimbali kwa Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Thobias Andengenye (katikati) alipotembelea ofisi hizo mapema leo asubuhi (wa pili kushoto) ni Mkurugenzi mkuu wa Shirika hilo Dk. Ayoub Rioba .
 Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji  Thobias  Andengenye aliyesimama mbele, akimsomea taarifa ya Jeshi hilo Mkurugenzi mkuu wa Shirika la Taifa la Utangazaji (TBC) Dk. Ayoub Rioba alipotembelea ofisi za Shirika hilo mapema leo asubuhi

 Kamishna Jenerali Thobias Andengenye (katikati) akipokea maelezo jinsi ya chumba cha matangazo kinavyofanya kazi (Studio) kutoka kwa Mtangazaji Bi Anna Mwasioke hayupo pichani, (kushoto) ni Mkurugenzi mkuu wa TBC Taifa Dk. Ayoub Rioba. Kwa picha zaidi BOFYA HAPA