Tatizo sugu la ugonjwa wa UTI na magonjwa ya ngozi yanayosabishwa na uchafu chooni, limepatiwa tiba baada ya kampuni ya Anuflo Industries Limited kuzindua karatasi maalum za kuzuia tatizo hilo lijulikanalo kwa jina la ‘Believe toilet seat cover’ ambazo huzuia maambukizi hayo.

Mbali ya karatasi hizo, kampuni hiyo pia imezindua karatasi maalum ya ‘kuondoa mafuta kwenye uso ijulikanayo kwa jina la “Believe blotting paper’ ambayo ni maalum kwa warembo, ma-bibi harusi na wanawake wenye tatizo hilo kwa ujumla.

Mkurugenzi Mtendaji wa Anuflo Industries Limited, Flora Christandus alisema kuwa ameamua kutengeneza bidhaa hizo kutokana na matatizo ambao yameanza kuwa sugu na kero kwa jamii.

Flora alisema kuwa tatizo la ugonjwa wa UTI na ugonjwa wa ngozi vimekuwa kero kubwa kwa jamii na hii inatokana na matumizi mabaya ya choo iwe nyumbani, kazini, sehemu za starehe na maeneo mengine kama Baa nk.

Alisema kuwa kuna watu si wastaharabu katika matumizi ya vyoo na usababisha kujisaidia haja ndogo kwenye sinki la choo na kumpa shida mtu mwenye lengo la kujisaidia haja kubwa.

“Inafikia hatua mtu anaamua kupanda juu ya sinki la choo ili kuepuka kukalia mkojo ambao umetokana na matatizo ya matumizi mabaya, matokeo yake ni uharibifu wa choo au kuhatarisha kuvunjika miguu kutokana na kuepuka ugonjwa wa UTI na magonjwa mengine ya ngozi,”

“Kwa kutambua tatizo hilo, tukaamua kuzalisha bidhaa hii ambayo inaingia sokoni kwa mara ya kwanza Tanzania tena kwa bei nafuu kuliko kutibu ugonjwa wa UTI ambao gharama yake ni kubwa na uhatarisha matatizo mbalimbali ya kiafya,” alisema Flora.

Alisema kuwa bidhaa hiyo itapatikana kwenye maduka ya Shear Illusions na kwenye supermarket mbalimbali za jijini na kuwaomba wadau kununua ili kujikinga na matizo hayo.Kuhusiana na karatasi maalum za kuondoa mafuta usoni, Flora alisema kuwa nazo zimeingia zenye ubora wa hali ya juu na kuondoa tatizo la mtu kujifuta kwa njia ya leso na ‘tissue’ ambazo si matumizi sahihi.

“Mabibi harusi, warembo na wanawake kwa ujumla,karatasi hizi ni sahihi kwa kuondoa mafuta usoni, tuache kutumia vitambaa, bidhaa hii imetengenezwa kwa ajili ya kuondoa tatizo hilo,” alisema.

Mkurugenzi Mtendaji wa Anuflo Industries Limited, Flora Christandus akimuelezea Afisa Mtendaji Mkuu wa Shear Illusions Shekha Nasser (wa pili kulia) jinsi ya matumizi ya karatasi maalum ya kutandika kwenye sinki la choo ijulikanyo kwa jina la Believe Toilet Seat cover mara baada ya uzinduzi wa bidhaa hiyo.Kushoto ni mmoja wa mdau wa bidhaa hiyo akishuhudia.

Afisa Mtendaji Mkuu wa Shear Illusions Shekha Nasser (katikati) akiitambulisha karatasi maalum ya kutandika kwenye sinki la choo ijulikanyo kwa jina la Believe Toilet Seat cover mara baada ya uzinduzi wa bidhaa hiyo. Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Anuflo Industries Limited, Flora Christandus na kushoto ni mmoja wa mdau wa bidhaa hiyo.

Mkurugenzi Mtendaji wa Anuflo Industries Limited, Flora Christandus wa pili kulia akimuelezea mmoja wa mdau, Shumbana Wawa ambaye anafanyakazi kampuni ya MultiChoice Tanzania, jinsi ya kutumia karatasi maalum ya kutandika kwenye sinki la choo ijulikanyo kwa jina la Believe Toilet Seat cover. Akifuatilia maelekezo hayo ni Afisa Mtendaji Mkuu wa Shear Illusions Shekha Nasser (wa pili kushoto) .

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Nawapongeza sana kwa kulifikiria hilo na kulitekeleza kwa vitendo na hatimae bidhaa kuwa sokoni. Pia nimesoma maelezo hapo kuwa ni..karatasi ya KUTANDIKA kwenye sinki la choo... Kwa nini wasitengeneze tu moja kwa moja "Anti-Bacterial WIPES" zenye scent/fragrance tofauti tofauti ambazo zitaondoa any sort of bacteria, grease na uchafu mwingineo wa aina yeyote katika hizo 'Toilet Seats' na arround the sink hilo la choo kwa jumla, ambazo zipo hygienic na toilet friendly (zenye kuwa flushed and disolve in the toilet) kama toilet paper za kawaida. (Hayo ni maoni yangu tu, sina lengo la kuikosoa bidhaa hiyo kwani ipo sahihi na kwa manusura yetu sisi wenyewe watumiaji wa vyoo hivyo husika).

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...