THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

Gadget

This content isn't available over encrypted connections yet.

DC KASESELA AKUTANA NA MASELA WA KIHESA, MJINI IRINGA, APIGA JALAMBA NA MGAMBO

Katika kupunguza kasi ya uhalifu na kuwawezesha Vijana wa Iringa, Mkuu wa wilaya ya Iringa, Richard Kasesela alikutana na vijana wa kijiwe cha Kihesa, ambao wengi wao wanajishughulisha na kuosha magari na kuwaomba kusaidiana naye katika kutokomeza udokozi.

Vijana hao walimuomba Mkuu wa Wilaya awasaidie upatikanaji wa mashine ya kuoshea magari ambayo aliwahidi kuwatafutia ndani ya siku 2 ili mradi wajiunge kwenye kikundi na wafungue akaunti benki. Vijana hao walimsukuru sana mkuu wa wilaya na kuahidi kuwa watiifu wa sheria na kuchapa kazi. Kikundi hicho kina vijana 25.
Mkuu wa wilaya ya Iringa, Richard Kasesela akifanya mazungumzo na Kikundi cha vijana 25 wanaojishughulisha na uoshaji wa magari katika eneo la Kihesa, Mjini Iringa.
Kasesela akipitia taarifa ya Kikundi hicho aliyokabidhiwa.
Akitoka eneo hilo baada ya kumaliza kuzungumza na vijana hao.


Kuna Maoni 2 mpaka sasa.

  1. Anonymous Anasema:

    Vijana walio vijiweni wawezeshwe kuona fursa zilizopo katika sekta mbali mbali ikiwemo ujenzi, kilimo, ujasiriamali, ili wasikae bure na kupoteza muda. Wengi wanahitaji kuhamasishwa na kuelezwa jinsi ya kujishughulisha katika mazingira waliyonayo na pengine mtaji mdogo ili wajitegemee.

  2. Anonymous Anasema:

    Umeongea vizuri sana mdau wa kwanza lakini kwa bahati mbaya si viongozi wala wahamasishaji wenye kuliona hilo, si ajabu ikawa ni mtaji kipindi cha uchaguzi.