Mkuu wa wilaya ya Iringa, Richard Kasesela alipokea wakina mama watatu wakiwa wanatetemeka kwa baridi, wakilalamika kumwagiwa maji ya baridi walipokuwa wamekaa kwenye eneo la kusubiria wagonjwa waliolazwa Katika Hospitali ya Rufaa Mkoani Iringa.

Akinamama hao wengi wao wametoka maeneo ya mbali na hospitali hiyo walimwagiwa na walinzi wa kampuni ya Amazon ambao ndio wamepewa kandarasi ya ulinzi hospitali ya Rufaa ya Iringa. 

Mkuu wa wilaya hiyo alifika hospitali kujionea hali halisi, baadae pia akapata taarifa kuwa jana yake Mlinzi wa kampuni hiyo alimpiga mzee aliyekuwa ameleta chakula katika hospitali hiyo na kumwaga kwa mateke. 

Mkuu wa wilaya aliamuru mlinzi huyo na mwenzake wakamatwe pia mwenye kampuni afike kituo cha polisi haraka iwezekanavyo. "Hali hii imeudhi sana hasa ukiona jinsi wakina mama walivyo nyanyasika wengine vyombo vyao na chakula kuloweshwa maji." alisema Mh Kasesela.
 Mkuu wa Wilaya ya Iringa, Richard Kasesela akitembelea katika jengo ambalo lililomwagwa maji na Mlinzi wa Kampuni ya Amazon Seculity na kuwaondoa akinamama walipokuwa wamekaa kwenye eneo la kusubiria wagonjwa waliolazwa Katika Hospitali ya Rufaa Mkoani Iringa.
Baadhi ya watu walioondoka eneo la kusubiri wagonjwa na kukaa nje katika hospitali ya Rufaa ya Mkoani Iringa. 
Eneo la Kupumzika watu nwanaoenda kuwaona wagonjwa katika hospitali ya Rufaa ya Mkoani Iringa likiwa limemwagwa maji.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Kama hayo yote yametendeka hao watu wapewe adhabu kali. Hawastahili kuwa sehemu kama hiyo ambapo kwanza kuuguliwa tu peke yake ni changamoto kubwa sana.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...