THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.


Gadget

This content isn't available over encrypted connections yet.

kufuatia mjadala wa kurudi kwa Mdau John Mashaka, Mdau Hildebrand Shayo aibuka

Ankal,
Nimeona nijitokeze ili kumuhakikishia mdau wa BLOG yetu pendwa aliyeomba mijadala yenye tija irudi hapa kwa manufaa ya kuelimishana.

Ni kweli wadau nikiri nilikutana na John Mashaka hivi majuzi (12/07/2016) katika uwanja wa ndege wa JK Nyerere na kati ya mazungumzo yetu kwa pamoja yalikuwa ni kwa namna gani tutashirikiana na wadau wa Globu hii ya Jamii kutoa mada zenye mshiko wa wafuatiliaji wa mambo mbali mbali yanayohusu Tanzania yetu.

Niwahakikishie kuwa muda si mrefu mtaanza kupata mijadala itayokuwa inaendana na “mwendo kasi” Tupo pamoja, niko Tanzania, na ninawashauri wale ambao mngependa kujua “utamu wa ngoma” njooni tuicheze wote.


Mdau
Hildebrand Shayo.

PS: Nashukuru sana Dr. Hildebrand Shayo na mdau John Mashaka kwa kujibu haraka matakwa ya wadau. Hii inaonesha ni jinsi gani Globu ya Jamii, inayotimiza miaka 11 ifikapo mwezi Septemba, inavyoendeleza Libeneke kwa kasi ile ile ya kuanzia kuzaliwa kwake kule Finlandia Hall, Helsinki, Finland. Sina cha kusema zaidi ya kuwakaribisha tena magwiji wa mijadala Dr. Shayo na mdau Mashaka. Mbarikiwe sana kwa kuendelea kuamini kwamba Globu ya Jamii iko pale pale na wadau wake.
- Ankal


Kuna Maoni 2 mpaka sasa.

  1. Anonymous Anasema:

    Dr. Shayo, kurudi kwenu kutanoga zaidi akiwepo gwiji au Genius wenu John Mashaka. Nadhani vijana mna chachu kubwa kuliongoza hili taiga, hasa hichi kizazi dizaini ya John Mashaka. Tunawasubiria sana na madaha zenu

  2. Anonymous Anasema:

    John Mashaka. Kauka, hapa watu wa wanatafuta Kiki Ile mbaya. Umaarufu wa mwenzao inakuwa dili. No Noma sana