Ankal,
Nimeona nijitokeze ili kumuhakikishia mdau wa BLOG yetu pendwa aliyeomba mijadala yenye tija irudi hapa kwa manufaa ya kuelimishana.

Ni kweli wadau nikiri nilikutana na John Mashaka hivi majuzi (12/07/2016) katika uwanja wa ndege wa JK Nyerere na kati ya mazungumzo yetu kwa pamoja yalikuwa ni kwa namna gani tutashirikiana na wadau wa Globu hii ya Jamii kutoa mada zenye mshiko wa wafuatiliaji wa mambo mbali mbali yanayohusu Tanzania yetu.

Niwahakikishie kuwa muda si mrefu mtaanza kupata mijadala itayokuwa inaendana na “mwendo kasi” Tupo pamoja, niko Tanzania, na ninawashauri wale ambao mngependa kujua “utamu wa ngoma” njooni tuicheze wote.


Mdau
Hildebrand Shayo.

PS: Nashukuru sana Dr. Hildebrand Shayo na mdau John Mashaka kwa kujibu haraka matakwa ya wadau. Hii inaonesha ni jinsi gani Globu ya Jamii, inayotimiza miaka 11 ifikapo mwezi Septemba, inavyoendeleza Libeneke kwa kasi ile ile ya kuanzia kuzaliwa kwake kule Finlandia Hall, Helsinki, Finland. Sina cha kusema zaidi ya kuwakaribisha tena magwiji wa mijadala Dr. Shayo na mdau Mashaka. Mbarikiwe sana kwa kuendelea kuamini kwamba Globu ya Jamii iko pale pale na wadau wake.
- Ankal

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Dr. Shayo, kurudi kwenu kutanoga zaidi akiwepo gwiji au Genius wenu John Mashaka. Nadhani vijana mna chachu kubwa kuliongoza hili taiga, hasa hichi kizazi dizaini ya John Mashaka. Tunawasubiria sana na madaha zenu

    ReplyDelete
  2. John Mashaka. Kauka, hapa watu wa wanatafuta Kiki Ile mbaya. Umaarufu wa mwenzao inakuwa dili. No Noma sana

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...