KUELEKEA ukingoni mwa Michuano ya kirafiki ya Kimataifa (ICC), Jioni ya leo ndani ya dimba la Wembley jijini London, takribani watazamaji 90,000 wanadhamiwa kukaa vitini kuutazama mtanange mkali wa kukata na shoka kati ya majogoo wa jiji Liverpool na mabingwa wa Laliga Fc Barcelona. Mpambano huu unawakutanisha mabingwa wa Ulaya mara 5 kila moja. 

Timu hizi mbili zimewahi kukutana katika mchezo wa kirafiki kama huu takribani miaka 40 iliyopita, zilikutana mwaka 1977 ndani ya dimba la Olympic Stadium, Amsterdam huko Uholanzi ambapo Liverpool wakiwa chini ya kocha Bob Paisley, walishinda kwa bao 1-0 lililofungwa na David Johnson.

Baada ya hapo timu hizi zimewahi kukutana tena mara sita katika mashindano ya Ulaya tangu mwaka 2001-2007, ambapo kila timu iliweza kupata ushindi mara mbili, kupoteza mara mbili na kutoka sare mara mbili. 
Tarehe 5/4/2001 timu hizi zilikumbana katika michuano ya Uefa Cup, Nou Camp, Barca wakiwa na magwiji kama Luis Enrique kocha wa sasa wa timu hiyo, Pep Guardiola, Patrick Kluivert na Rivaldo, huku Liver ikiwa na nyota kama Robbie Fowler, Steve Gerard na Michael Owen. Timu hizi hazikuweza kufungana.

Tarehe 19/4/2001, kwenye Uefa Cup huko Anfield Liverpool wakapata ushindi wa bao 1-0, bao lililofungwa na Gary McAllister. Lakini mwaka huo huo 2001 November 20 katika uwanja wa Nou Camp Barcelona wakailaza Liverpool kwa mabao 3-1, Liver walianza kwa bao la Michael Owen lakini Barca wakapata mabao yao kupitia kwa Kluivert, Overmass na Rochemback. 2002, March13, kwenye Champions league huko Nou Camp timu hizi hazikuweza kufungana.

Februari 21-2007 katika michuano ya Champions League ndani ya dimba la Camp Nou wenyeji Barcelona walilala kwa mabao 2-1 kutoka kwa Liverpool kwa mabao ya Craig Bellamy na John Arne Riise huku Deco akiifungia Barcelona bao la kufutia machozi.
Mwisho ilikuwa 2007, March 6, katika uwanja wa Anfield kwenye michuano ya Champions League Liverpool ililala dhidi ya Barcelona kwa bao 1-0, goli ambalo lilifungwa na Eidur Gudjohnsen. Wakati huo Barcelona walikuwa wamesheheni wakali kama vile Samwel Eto'o, Ronaldinho na Lionel Messi.

Kivutio kikubwa katika mchezo huu ni urejeo wa mchezaji Luis Suarez alijiunga na Barcelona akitokea Liverpool huku akiwa ni kipenzi cha mashabiki wa timu hiyo, swali ni je atapokewa vipi?

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...