Mashirika ya kiraia na serikali kwa pamoja yametakiwa kushirikiana na kuratibu shughuli zake kwa ukaribu kushughulikia matatizo na migogoro ya ardhi kwa ufanisi mkubwa.

Hayo yameelezwa na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi mjini Morogoro, katika mkutano wa siku mbili uliozikutanisha Tume ya Taifa ya Mpango wa Matumizi ya Ardhi, iliyo chini ya wizara ya Ardhi na asasi mbalimbali ambazo zenye kujishughulisha na masuala ya ardhi.

Mkutano huo uliohudhuriwa pia na mkuu wa mkoa wa Morogoro, Steven Kebwe, uliangalia mpango wa taifa wa matumizi ya ardhi na mchango wake katika kupunguza migogoro ya archi nchini Tanzania.

Vilevile mkutano huo ulijadili na kuangalia changamoto zilizopo katika masuala ya ardhi hasa upimaji, mipango ya matumizi ya ardhi, na ushiriki wa wananchi wa vijijini hasa wanawake katika utatuzi wa masuala matatizo ya ardhi.

Waziri Lukuvi, alisisitiza kuwepo kwa uratibu wa pamoja shughuli za wadau wa ardhi ili kuwa na dira itakayowezesha utatuzi wa haraka wa matatizo ya ardhi.
Waziri Lukivi amesema jambo hilo litawesesha wadau wa ardhi kufanya uamuzi wa tija katika maamuzi ya sehemu za kwenda zenye migogoro ardhi na kuwafikia wananchi wote.

Mkutano huo uliokutanisha watendaji wa serekali na mashirika ya kiraia, uliandaliwa na Tume ya Taifa ya Mpango wa Matumizi ya Ardhi, CARE International Tanzania, OXFARM, na Tanzania Resources Forum.
Meza kuu kutoka kushoto Mkurugenzi wa programu ya Maliasiai wa Care International Tanzania Thabit Masoud, Mkurugenzi wa Tume ya Taifa ya Mpango wa Matumizi ya Ardhi Dr Steven Nindi, mkuu wa mkoa wa Morogoro Steven Kebwe, Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi, na Kamishna wa ardhi Bi Mary Makonda.
Mkurugenzi wa Tume ya Taifa ya Mpango wa Matumizi ya Ardhi Dr Steven Nindi akitoa mada kwa washiriki wa mkutano huo.
Mratibu wa mradi wa Ardhi Yetu wa shirika la CARE International Tanzania, Bi Mary Ndaro, akitoa mada katika mkutano.
Mkurugenzi wa programu ya Maliasili wa Care International Tanzania, Thabit Masoud akitoa mada kwa washiriki.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...