Balozi wa Uganda nchini Tanzania Bi. Dorothy Samali Hyuha akisaini kitabu cha maombolezo na kutoa salamu za rambirambi kufuatia kifo cha aliyekua Rais wa Pili wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mzee Aboud Jumbe Mwinyi.
 Mwakilishi wa Ubalozi wa Nigeria nchini Bi. Abiola Sherif Deluya akitoa salamu za pole katika kitabu maalumu kilichopo katika Ofisi ya Makamu wa Rais Mtaa wa Luthuli, Jijini Dar es Salaam leo.
Balozi wa Palestina Mheshimiwa Hazim Shabat ni miongoni mwa mabalozi waliotembelea Ofisi ya Makamu wa Rais leo na kutoa salamu za pole kufuatia kifo cha aliyekuwa Rais wa Awamu ya Pili wa Zanzibar.
Balozi wa Kuwait nchini Tanzania Bw.  Jassem Al Najem ni miongoni mwa mabalozi waliotembelea Ofisi ya Makamu wa Rais leo na kutoa salamu za pole kufuatia kifo cha aliyekuwa Rais wa Awamu ya Pili wa Zanzibar. Picha zote na Ofisi ya Makamu wa Rais

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...