Na Frank Mvungi- Maelezo.
Madawati
30,000 mbioni kukamilika ili yaweze kusambazwa katika Mikoa na Halmashauri zote
hapa Nchini ikiwa ni utekelezaji wa awamu ya pili ya mpango wa Serikali wa
kutengeneza madawati elfu 60 kwa ajili ya shule za Msingi na Sekondari hapa
nchini.
Kauli hiyo
imetolewa Leo jijini Dar es salaam na Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga
Taifa Mhe. Dkt. Hussein Mwinyi wakati wa mkutano na
waandishi wa habari.
Akifafanua
Dkt. Mwinyi amesema kuwa katika awamu ya pili madawati 20,000 yameshakamilika na yanaweza kuchukuliwa
kuanzia sasa kwenda kwenye majimbo yaliyopangiwa kupata madawati hayo.
“Madawati
elfu kumi yaliyobaki yatakamilika wakati wowote kabla ya muda wa mwisho
uliowekwa”Alisisistiza Dkt. Mwinyi.
Katika
kutekeleza mpango huo, awamu yakwanza jumla ya madawati 32,387 yalitengenezwa
na yaliyochukuliwa na Wabunge kwa kushirikiana na Halmashauri zao ni 22,721
tu,hivyo madawati 9,666 sawa na asilimia 30% bado hayajachukuliwa na Majimbo
husika.
Akitaja
Baadhi ya Mikoa iliyonufaika na Madawati hayo Dkt. Mwinyi amesema kuwa ni Tanga
madawati 6444, Njombe 3222,Iringa 3709, Mbeya 3759, Songwe 3222, Rukwa 1611,
Ruvuma 4833,Visiwa vya Unguja 3200,Pemba 1800.
Akizungumzia
Majimbo ambayo hayajachukua madawati yake katika awamu ya kwanza Dkt.Mwinyi
amesema ni vyema Viongozi katika Majimbo hayo wakiwemo Waheshimiwa Wabunge wanatakiwa
wakachukue madawati hayo kabla ya mwisho wa mwezi huu.
Majimbo
ambayo hayajachukua madawati yake katika awamu ya kwanza yametajwa kuwa ni Kilindi,Pangani,Makambako,Ludewa,Wangingombe
naMakete..
Majimbo mengine
ni Kyela,Rungwe,Busokelo,Songwe,Kwela,Tunduru,Iringa Mjini,Mbeya Mjini,Mbeya
Vijijini na Ileje Nkasi Kaskazini na Nkasi Kusini.
Tarehe 11
April,2016 Serikali ilitoa zabuni kwa JKT kutengeneza madawati 60,000 kwa
gharama ya Bilioni 3 ambapo bei ya kila dawati ni sh 50,000/,aidha tarehe 13
Julai 2016 JKT ilikabidhi madawati 32,387.
Waziri
wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Mhe. Dkt. Hussein Mwinyi akizungumzia
utekelezaji wa awamu ya pili ya mpango wa kutengeneza madawati 30,000
unaotekelezwa na JKT ili kukamilisha madawati 60,000 yaliyopangwa na
Serikali hali itakayosaidia kuondoa tatizo la madawati katika shule za Msingi
na Sekondari hapa Nchini.
Mkuu wa
Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) Brigedia Jenerali Michael Isamuhyo akifafanua kwa
waandishi wa Habari leo jijini Dar es
salaam kuhusu Ubora wa madawati yaliyotengenezwa na JKT na kusisitiza kuwa yana
ubora unaotakiwa ambapo madawati hayo ni sehemu mpango wa serikali kukabiliana
na changamoto ya upungufu wa Madawati
hapa Nchini.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...