WALEMAVU 19 wametunukiwa vyeti vya kuhitimu mafunzo ya udereva ya mwezi mmoja kutoka katika shule ya udereva ya Nyato’s kilichopo Majohe Manispaa ya Ilala, Jijini Dar es salaam huku Mkuu wa Usalama mkoa wa kipolisi wa Ilala, Mrakibu Msaidizi wa Polisi (ASP) Peter Mashishanga akiwataka kabla ya kuingia barabarani wahakikishe wanakwenda kufanyiwa maribio ili kuweza kupata leseni.

Akizungumza katika Hafla fupi ya kukabidhi vyeti hivyo iliyofanyika chuoni hapo Majohe Wilayani Ilala, Mashishanga alisema anaamini wahitimu hao watakwenda kuwa mabalozi wazuri kwa wengie hususani wale ambao hawafuati sharia na kuamua kuingia barabarani pasipo kupata hata mafunzo wala leseni.

“Leo hii mmepata vyeti hivi ni hatua muhimu ila sasa kabla hamjaaza kuendesha lazima mje pale Polisi katika Ofisi za Kikosi cha Usalama barabarani ili kuweza kujaribiwa na wakufunzi wetu tayari kwa kupata leseni itakayowapa ruksa ya kutumia vyombo vyenu vya moto”alisema.

Naye Mkurugenzi wa shule hiyo, Wilfred Nyato alishukuru kwanamna anavyoshirikiana na Kikosi hicho huku akiahidi kuendelea kufanya kazi kwa pamoja na pia alimweleza Mkuu huyo wa Usalama wa mkoa wa kipolisi kuwa shule yake imetoa Ofa ya kusoma bure kwa mlemavu Thomas Kone ambaye hivi karibuni alipata msaada wa bajaji kutoka kwa Rais Dkt. John Magufuli.
Mkuu wa Usalama Barabarani mkoa wa kipolisi Ilala, Mrakibu Msaidizi (ASP), Peter Mashishanga akikabidhi cheti kwa,Mussa Nyahove leo jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Usalama Barabarani mkoa wa kipolisi Ilala,Mrakibu Msaidizi (ASP)Peter Mashishanga akizungumza na wahitimu wa mafunzo ya udereva ya mwezi mmoja kutoka katika Chuo cha udereva ya Nyato’s kilichopo Majohe Manispaa ya Ilala jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Chuo hicho, Wilfred Nyato akimkaribisha Mkuu wa Usalama Barabarani mkoa wa kipolisi Ilala,Mrakibu Msaidizi (ASP)Peter Mashishanga kuongea machache na wahitimu hao leo jijijni Dar es Salaam.
Mkuu wa Kitengo cha Elimu kwa Umma Jeshi la Polisi,  Mrakibu Msaidizi (ASP) Mossi Ndozero akitoa elimu kwa wahitimu wa mafunzo ya udereva ya mwezi mmoja kutoka katika Chuo cha udereva cha Nyato’s kilichopo Majohe Manispaa ya Ilala jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mkuu wa Usalama Barabarani mkoa wa kipolisi Ilala, Mrakibu Msaidizi (ASP), Peter Mashishanga.
Mkuu wa Usalama Barabarani mkoa wa kipolisi Ilala, Mrakibu Msaidizi (ASP), Peter Mashishanga akiwa katika picha ya Pamoja na wahitimu wa mafunzo ya udereva ya mwezi mmoja kutoka katika Chuo cha udereva cha Nyato’s kilichopo Majohe Manispaa ya Ilala jijini Dar es Salaam leo.(Picha na Emmanuel Massaka, Globu ya Jamii)

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...