Mgeni Rasmi, Jaji Mkuu wa Zanzibar, Mhe. Omar Othman Makungu leo akifungua rasmi mafunzo ya siku tatu kuhusu Miongozo ya Luanda juu ya taratibu za ukamataji na ushikiliaji wa watuhumiwa kabla ya kufunguliwa mashtaka. Mafunzo hayo yanafanyika Zanzibar Beach hotel mjini Zanzibar na yanawashirikisha takriban maafisa 50 wa Jeshi la Polisi, Magereza, Vyuo vya Mafunzo, Mahakama na Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora kutoka Tanzania Bara na Visiwani Zanzibar.
 Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB), Mhe. Bahame Tom Nyanduga akitoa neno la utangulizi kabla ya kumkaribisha Mgeni Rasmi, Mhe. Jaji Mkuu wa Zanzibar kutoa hotuba yake ya ufunguzi.
 Meneja Miradi kutoka taasisi ya African Policing Civilian Oversight Forum (APCOF) yenye makao yake nchini Afrika Kusini, Bi. Louise Edwards akiongea wakati wa ufunguzi wa mafunzo kuhusu Miongozo ya Luanda yaliyoanza leo mjini Zanzibar.
Mgeni Rasmi, Jaji Mkuu wa Zanzibar, Mhe. Omar Othman Makungu (katikati) na Mwenyekiti wa THBUB, Mhe. Bahame Tom Nyanduga (wa pili kushoto) wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya washiriki wa mafunzo kuhusu Miongozo ya Luanda (Luanda Guidelines on the conditions of arrest, police custody and pre–trial detention in Africa) yaliyoanza leo Zanzibar Beach Hotel mjini Zanzibar. Wengine waliokaa kutoka kushoto ni: Katibu Mtendaji wa THBUB, Bibi Mary Massay, Mwakilishi kutoka taasisi ya African Policing Civilian Oversight Forum – APCOF, Bi. Louise Edwards na Kaimu Kamishna wa Jeshi la Polisi Zanzibar, Bwana Azizi Juma. Mafunzo hayo yameandaliwa THBUB kwa ushirikiano na taasisi ya APCOF ya Afrika Kusini. Kupata hotuba ya ufunguzi BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...