Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia kwenye ufunguzi wa mkutano wa mwaka wa Wakadiriaji Majenzi kutoka Afrika uliofanyika kwenye Hotel ya Golden Tulip jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa akihutubia kwenye mkutano wa mwaka wa Wakadiriaji Majenzi kutoka Afrika.
Rais wa Chama Cha wakadiriajiMajenzi Afrika Prof. Robert Pearl akihutubia mkutano wa Wakadiriaji Majenzi uliofanyika kwenye hotel ya Golden Tulip.
Sehemu ya wajumbe waliohudhuria mkutano huo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza jambo na Viongozi wa Chama cha Wakadiriaji majengo mara baada ya kufungua mkutano wa mwaka wa Wakadiriaji Majenzi kutoka Afrika uliofanyika kwenye Hotel ya Golden Tulip jijini Dar es Salaam.
.......................................

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amewataka wakadiriaji majenzi nchini wahakikishe wanafanya kazi kwa kuzingatia maadili na waepuke vitendo vya rushwa katika mchakato wa ukadiriaji majengo nchini.Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan ametoa kauli hiyo 18-Aug-16 wakati anafungua mkutano wa mwaka wa wakadiriaji majenzi kutoka nchini mbalimbali za Afrika jijini Dar es Salaam.

Makamu wa Rais amesisitiza kuwa kwa sasa serikali ipo kwenye mchakato wa kuanza kutekeleza miradi mikubwa ya kiuchumi ikiwemo ujenzi wa reli ya kati kwa kiwango cha kisasa (Standard gauge) na ujenzi wa bomba la mafuta kutoka nchini Uganda hadi Tanga, Tanzania na suala la kuhamia Makao Makuu Dodoma hivyo ni muhimu kwa wakadiriaji majenzi wakajipanga vizuri katika utekelezaji wa miradi hiyo mikubwa kwa kuweka gharama nafuu kulingana na hali halisi ya mradi unaotakiwa kujengwa.

Amesema serikali inatambua mchango wa watalaamu wa ukadiriaji majenzi hivyo ni muhimu kwa wataalamu hao wakauongeza bidii katika utekelezaji wa kazi zao hasa kwa kuzingatia teknolojia za kisasa.Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan amehimiza ushirikiano kati wakadiriaji majenzi wa Tanzania na wa nchi nyingine za Afrika katika kubadilishana uzoefu kwenye kazi zao ili kuongeza ubunifu na ufanisi katika miradi wanayopata.

Kwa upande wake Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa amesema serikali imetenga dola bilioni 2.4 kwa ajili ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwemo ujenzi wa barabara, madaraja na bandari na viwanja wa ndege hivyo serikali inahitaji wakadiriaji majenzi waadilifu katika utekelezaji wa miradi hivyo na sio vinginevyo.

BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...