Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amewahimiza viongozi wa mkoa wa Lindi wasimamie kikamilifu zoezi la utengenezaji wa madawati ili kuhakikisha madawati yanayotengenezwa yanakuwa na ubora na yanakidhi viwango vinavyotakiwa.

Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan ametoa kauli hiyo mjini Lindi Tarehe 7-Aug-2016 katika mkutano wake na wajasiriamali wa mkoa Lindi pamoja na viongozi mbalimbali wa mkoa huo.

Makamu wa Rais amesema msukumo mkubwa wa serikali uliopo kwa sasa unalenga kuhakikisha madawati yanayotengenezwa kote nchini yanakuwa imara huku akipongeza jitihada kubwa zinazofanywa na serikali ya mkoa wa Lindi ya utengenezaji wa madawati ambapo mpaka sasa mkoa huo umebakisha asilimia Moja tu ya utengenezaji wa madawati hayo ili kukamilisha zoezi hilo.

Kuhusu mikopo kwa wajasiriamali, Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan amesisitiza kuwa serikali italifanyia kazi ombi la wajasiriamali wa mkoa wa Lindi ambao wameiomba serikali ifanye mazungumzo na watendaji wa taasisi za kifedha nchini ili waweze kupunguza riba kwenye mikopo wanayopata kama hatua ya kuongeza hamasa kwa wananchi wengi zaidi kukopa fedha kwa ajili ya kuimarisha shughuli ujasiriamali.

Makamu wa Rais pia amezitaka halmashauri zote nchi kutekeleza kwa vitendo mkakati wa kutenga asilimia TANO ya makusanyo ya mapato yake na kutoa fedha hiyo kwa wanawake na vijana kwenye halmashauri hizo ili waweze kuanzisha na kuendeleza miradi yao ya kiuchumi kwenye maeneo yao.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia Wajasiriamali wa mkoa wa Lindi kwenye ukumbi wa Kanisa Katoliki la Mtakatifu Kagwa.
Mkuu wa mkoa wa Lindi Ndugu Godfrey Zambi akisoma taarifa ya mkoa wakati wa mkutano uliowakutanisha Makamuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Wajasiriamali wa mkoa wa Lindi katika ukumbi wa Kanisa Katoliki la Mtakatifu Andrea Kagwa.
Wajasiriamali wa mkoa wa Lindi waliohudhuria mkutano wao na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...