THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

Gadget

This content isn't available over encrypted connections yet.

MAKATIBU WAKUU WATEMBELEA KITUO MAHIRI CHA KUTUNZA KUMBUKUMBU (INTERNET DATA CENTRE) KIJITONYAMA DAR ES SALAAM

 Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano anayeshughulikia sekta ya Mawasiliano Dkt. Maria Sasabo akitoa maelezo ya kituo mahiri cha kutunza kumbukumbu (internet Data Centre) kwa Makatibu Wakuu hawapo pichani walipotembelea kituo hicho kilichopo eneo la Kijitonyama DSM. 
Afisa kutoka Kampuni ya Simu Tanzania TTCL Bw. Suleimani Kagobe  akitoa maelezo kwa Makatibu Wakuu jinsi mfumo wa umeme unavyofanya kazi walipotembelea katika kituo mahiri cha kutunza kumbukumbu kilichopo eneo la Kijitonyama DSM. 
Katibu Mkuu wa Wizara  ya  Ardhi Dkt. Yamungu Kayandabila   katikati akitoa   maoni  yake kuhusu  kituo mahiri cha kutunza kumbukumbu “ internet Data Centre”,  (wa kwanza kulia) ni Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya nje na Afrika Mashariki Balozi Ramadhani Mwinyi na (wa kwanza kushoto) ni Kaimu Katibu Mtendaji wa Tume ya Mipango Bibi Florence Mwanri walipokitembelea kituo hicho eneo la Kijitonyama DSM. Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano .