Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda amemtaka Mkurugenzi wa jiji kuanza  mchakato wa kuhamisha kituo kikuu cha mabasi ya mkoani cha ubungo  kuhamia Mbezi mwisho 

Makonda ameyasema hayo leo wakati alipotembelea  kituo hicho leo, amesema kituo hicho kimeelemewa na idadi ya kubwa ya wasafiri huku miundombinu haiendani na utoaji wa huduma kwa wasafiri wanaotumia kituo hicho.


Makonda  amesema kuwa baada ya kituo hicho kuhama panatakiwa kufanyika  uwekezaji wa soko kubwa  ili kupunguza msongamano wa watu katika soko la Kariakoo.

Aidha Makonda amesema kuwa uamuzi huo umetokana na kuonekana kwa kituo hicho kuwa kidogo na kushindwa kutoa huduma ya usafirishaji ya abiria wanaoingia na kutoka katika mikoa mbalimbali.


Makonda ameutaka uongozi wa kituo hicho  kufunga taa maeneo yote kutokana na kutawala kwa giza nyakati za  usiku,ambapo ni  hatari kwa usalama wa abiria  wanaoshuka  nyakati hizo.

RC Makonda pia amepiga marufuku kukamata magari kwa kigezo cha maegesho, wakati hakuna alama zinazoonyesha sehemu ya kuegesha magari.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda akitembelea Kituo kikuu Ubungo cha Mabasi yaendayo mikoani na nchi jirani, leo.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda akizungumza na sehemu ya Wananchi waliokuwepo kwenye Kituo Kikuu cha Ubungo, Jijini Dar es salaam leo.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda akiwasalimia wananchi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Hongera kwa uamzi huo wa tija. Hicho kituo kipya kiwe cha kisasa. Litengwe eneo la kujenga migahawa. Ofisi ziwe za kisasa. Watu wanunue tiketi bila kuhusisha wapiga debe. Kituo kiwe na taa za kutosha na usalama wa kutosha. Ziwepo hostel karibu kwa ajili ya wageni wanaofika usiku toka nchi za jirani. Kweli kiwe kituo cha kuvutia biashara. Ushauri wa pili kwa mkuu wa mkoa. Inatia aibu kuingia Jijini Dar bila kujua kama umeingia Dar hasa wakati wa usiku. Nashauri mipaka ya Dar tokea bagamoyo, morogoro na mbagala kuwepo na mabango makubwa yenye baadhi ya picha za Dar es Salaam. Usiku yawe yanawaka. Ziwekwe taa za kumulika usiku walao kwenye mwanzo wa mpaka. Ili iwe ni ishara kuwa sasa unaingia Dar. Mabango madogo yaliyopo yanasomeka mchana tu na ni madogo. Wanaoingia Dar usiku hawawezi kujua kama wameingia Dar. Nafikiri kuna haja kuweka mabango makubwa ya kulitangaza na kuvutia biashara. Mtu akianza kuingia Dar ajue kweli ameingia Dar. Kwa sasa watu wanaingia Dar na giza. Wanachungulia kujua waliko na hawawezi. Ni giza tupu. Kuwepo mkakati wa kuhamasisha halimashauri na vitongoji vyake viweke taa za kuwaka usiku. Mji uwake upendeze. Namna hiyo tutavutia wageni wengi kuja kuwekeza na kuishi Dar. Mapato ya kodi yataongezeka. Tuipambe miji yetu ipendeze. Usiku ing'are. Tuweke taa nyingi kadiri tuwezavyo. Tutaona matokeo yake. Mitaji itakua mara dufu maana watu wataipenda miji yetu. Hongera Makonda na hili najua kwa kushirikiana na mkurugenzi na Mameya mtaliweza. Huu ndio wakati wa kuipamba Dar.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...