HABARI zilizotufikia zinasema kuwa Mwenyekiti wa Yanga Yusuf Manji, amejiuzulu wadhifa wake wa kuiongoza Yanga na kuamua kukaa pembeni.

Mbali na kujiuzulu huko pia imeelezwa na chanzo cha uhakika kutoka ndani ya Klabu hiyo, kuwa Mwenyekiti huyo pia ameamua kusitisha lengo lake la kuimiliki Yanga na Nembo yake ili kuiendesha kibiashara.

''Endapo maamuzi ya Mwenyekiti huyo yatakuwa ni kama zilivyoenea habari katika baadhi ya mitandao basi litakuwa ni pigo kubwa sana kwa wanayanga, waliokwisha jenga imani kubwa kwa Mwenyekiti huyo''. alisema shabiki mmoja wa Yanga. 

Aidha imeelezwa kuwa chanzo cha Manji kujitoa Yanga ni pamoja na figisu figisu za baadhi ya viongozi wa Serikali zinazomshutumu na baadhi ya Wananchama wa Yanga wasio kubari mageuzi anayotaka kuyafanya ndani ya Klabu hiyo, ambao wengi wao wanadaiwa kutumiwa na baadhi ya wafanyabiashara. 
Miongoni mwa watu wanaoweza kuwa kichwani mwa Mwenyekiti huyo hadi sasa pia anaweza kuwepo Katibu wa Baraza la wazee Mzee Akili Mali, aliyesikika katika mahojiano na moja ya kituo  cha Radio akimshutumu Mwenyekiti wake 'eti kuwa amekurupuka' kutaka kuichukua timu yao.

Manji anaonekana kuchoshwa na tabia za baadhi ya watu kumtukana na kumkebehi kwa hatua yake ya kuichukua timu ya Yanga na sasa ameamua kukaa pembeni kulinda heshima yake.
Hata hivyo viongozi wa Secretarieti ya Yanga leo wameonekana kuchanganyikiwa huku baadhi wakiwa wanapigana vikumbo kuingia na kutoka Ofisi za Manji zilizopo Quality plaza.
Huko Klabuni nako hali si hali, Baadhi ya WanaYanga wamefurika nje ya Jengo la Yanga, lililopo kwenye makutano ya Mtaa wa Twiga na Jangwani kutaka kujua hatma ya Kiongozi wao huyo waliemchagua kwa kura nyingi hivi karibuni. Globu ya jamii inaeendelea kufatilia segere hili kwa ukaribu na tutaendelea kupeana taarifa zaidi hapo baadae.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...