THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

Gadget

This content isn't available over encrypted connections yet.

MAREHEMU BI SHAKILA KUZIKWA LEO SAA 10 MBAGALA CHARAMBE JIJJINI DAR ES SALAAM


Kwa mujibu wa familia marehemu Bi. Shakila Saidi anatarajiwa kuzikwa leo Jumamosi Agosti 20, 2016 saa 10 alasiri katika makaburi ya Uwanja wa Ninja huko Mbagala Charambe jijini Dar es salaam  

Namna ya kufika msibani nyumbani kwa marehemu kwa kutumia daladala. Unapanda magari ya Mbagala Rangi Tatu, ukifika mwisho unachukua basi la Nzasa na unashuka Mnara wa Voda hapo unauliza kwa Bi Shakila utaonyeshwa.

Bi Shakila alifariki jana baada ya kuanguka nyumbani kwake mara baada ya kuswali swala ya Magharibi. Kwa mujibu wa binti yake, Shani, mkongwe huyu wa taarabu hakuwa anaumwa wajati mauti yanamkuta.

KALALE PEMA PEPONI KIPENZI CHETU BI. SHAKILA


Kuna Maoni 3 mpaka sasa.

 1. HK Anasema:

  MOLA akulaze pema Peponi Kipenzi chetu Bi Shakila Saidi. Amen.

 2. Anonymous Anasema:

  Hivi hakuna picha ambazo aliwahi kujistiri mkaweka kaka michuzi eeh!

 3. Anonymous Anasema:

  Umeuliza la maana mdau wa 2. Mini nadhani hawa wanahabari wetu wanahitaji mafunzo zaidi katika fani yao hiyo ya habari maana ni muhimu kujuwa picha ya aina gani inaendane na habari gani na mazingira gani, hilo bado ni tatizo, mana wanaweza kuweka picha ikamdhalilisha muhusika bila wao kujali.

  Pumzika kwa amani Pema Peponi Daima Milele Bi Shakila Saidi. Amin.