Muigizaji Maarufu wa sanaa ya vichekesho kutoka kundi la Orijino Komedi, Emmanual Mgaya a.k.a Masanja Mkadamizaji akishuhudia sebene babkubwa lililokuwa likiporomoshwa na Mkewe Bi. Monica Masatu alikuwa sambamba na Muigizaji mwenzake katika kundi hilo, Isaya Mwakilasa a.k.a Wakuvwanga, katika hafla ya Ndoa yao iliyofanyika jana kwenye ukumbi wa Primrose, jijini Dar es salaam.Picha zote na Joseph a.k.a Kasampaidadaily
Masanja Mkadamizaji akizungumza jambo huku Mkewe Monica Masatu akisikiliza.
 Moja ya vitu vilivyowavutia watu wengi walioalikwa kwenye mnuso huo, ilikuwa ni hii show ya wakali hawa wa kuvunja mbavu ambao ni wafanyakazi wenza wa bwana harusi kutoka kundi la Orijino Komedi yaani hapo namzungumzia Joti, Wakuvwanja na Profesa. hawa jamaa waliiteka kabisa sherehe hiyo.

BOFYA HAPA KUONA PICHA ZAIDI

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Hiyo mikanda (katika vazi mfano wa Polisi nchini) hivi huwa inafungwa tu almuradi au inakuwa na ufungaji unaozingatia mpangilio wa rangi, yaani rangi ipi iwe kwa juu na ipi iishie chini (Kijani-Bluu/Bluu Kijani) mfano bendera yetu ya Taifa inaanza na Kijani na kuishia na Bluu na sio Bluu kuishia Kijani. Japo ni 'Commedy' lakini alama za Taifa popote zinapoonekana kutumika au kuwepo basi ni lazima zipewe heshima yake au zitumike inavyostahili. Ni maoni yangu kama hilo limefahamika.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...