Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kulia) akimkabidhi mpira Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani nchini, Naibu Kamishna, Mohamed Mpinga ikiwa ni ishara ya Naibu Waziri huyo kuzindua Mashindano ya Mpira wa Miguu kwa Waendesha Pikipiki katika Mkoa wa Kipolisi wa Ilala, jijini Dar es Salaam. Mashindano hayo yajulikanayo kwa jina la Mpinga CUP yanatarajiwa kuanza kesho jijini humo. Katika hotuba yake, Masauni aliwataka waendesha Boda Boda jijini humo na nchini kwa ujumla kufuata sheria za usalama barabarani, na pia elimu ambayo wanapewa waitumie vizuri ili kuepuka ajali mbalimbali zinazosababishwa na uzembe wa madereva hao.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni akizungumza na waendesha Pikipiki/Boda Boda (hawapo pichani) kabla ya kuzindua Mashindano ya Mpira wa Miguu kwa Waendesha Pikipiki katika Mkoa wa Kipolisi wa Ilala, jijini Dar es Salaam. Mashindano hayo yajulikanayo kwa jina la Mpinga CUP yanatarajiwa kuanza kesho jijini humo. Katika hotuba yake, Masauni aliwataka waendesha Boda Boda jijini humo na nchini kwa ujumla kufuata sheria za usalama barabarani, na pia elimu ambayo wanapewa waitumie vizuri ili kuepuka ajali mbalimbali zinazosababishwa na uzembe wa madereva hao. Kushoto ni Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani nchini, Naibu Kamishna, Mohamed Mpinga. Kulia ni Wafadhili wa Mashindano hayo.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (aliyevaa koti) akimsikiliza Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani nchini, Naibu Kamishna, Mohamed Mpinga wakati alipokuwa anazungumza na Waendesha Boda Boda (hawapo pichani), kabla ya Naibu Waziri Masauni kuzindua Mashindano ya Mpira wa Miguu kwa Waendesha Pikipiki katika Mkoa wa Kipolisi wa Ilala, jijini Dar es Salaam. Katika hotuba yake, Kamanda Mpinga alisema Mashindano hayo ambayo yameshirikisha Wilaya za Temeke, Kinondoni na sasa Ilala yanatarajiwa kumalizika Septemba 18, 2016. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...