CHAMA cha chezo wa Pool Mkoa wa Dar es Salaam kimeaandaa mashindano ya Pool katika kusheherekea siku kuu ya nanenane yatakayofanyika katika Viwanja vya TCC Chang’ombe jijini Dar es Salaamyajulikanayo kama “88” Pool Competitions 2016.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, mratibu wa mashindano hayo, Michael Machellah alisema maandalizi yako vizuri kwani mpaka sasa mikoa 12 imeshathibitisha kushiriki ikiwakilishwa na baadhi ya vilabu vyake.

Alisema Machellah mikoa hiyo ni pamoja na Mkoa wa Dodoma, Morogoro,Iringa,Mbeya,Pwani,Tanga,Kilimanjar o,Arusha,Manyara,Mkoa wa kimichezo wa Ilala, Mkoa wa kimichezo wa Kinondoni na Mkoa wa kimichezo wa Temeke ambao ndio wenyeji wa mashindano hayo.

Mashindano yao yanatarajiwa kuanza rasmi Alhamis tarehe 4 Agosti 2016 na kumalizika siku ya siku kuu ya nane nane tarehe 8 Agost 2016. Zawadi katika mashindano hayo, Bingwa upande wa timu ataibuka na Kashi shilingi laki tano na kikombe, msindi wa pili 250,000/-, mshindi wa tatu 150,000/- na mshindi wa nne ni 50,000/-.

Upande wa mchezaji mmoja mmoja Bingwa atazawadiwa Shilingi 200,000/-, wa pili shilingi 100,000/-, mshindi wa tatu 50,000/- na wan ne ni shilingi 25,000/-.

Mwisho aliwaomba wadau na wapenzi wa mchezo wa pool kujitokeza kuja kushuhudia mashindano hayo katika Viwanja vya TCC Chang’ombe jijini Dar es Salaam.
Mratibu wa mashindano ya Pool ya nane nane( “88” Pool Competition 2016), Michael Machellah (kushoto) akiwakabidhi Mwenyekiti wa Chama cha waamuzi wa mchezo huo, Hashim Sheweji(kulia) na Bingwa wa Afrika wa mchezo huo 2014, Patric Nyangusi, kikombe cha mshindi wa kwanza wa mashindano hayo yanayotarajiwa kuanza kesho katika viwanja vya TCC Chang’ombe Mkoani Dar es Salaan.Picha Prona Momwi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...