Mchezaji  Faraja Malaki wa Tanzania akiwania mpira mbele ya Wachezaji wa Uganda katika michezo wao wa Kwanza wa mashindano ya Majeshi kwa nchi za  Afrika Mashariki katika Uwanja wa Amahoro Nchini Rwanda Tanzania ilishinda 29-27 .
 Mchezaji  Veronica Patrick wa Tanzania akiwania mpira mbele ya Wachezaji wa Uganda katika michezo wao wa Kwanza wa mashindano ya Majeshi kwa nchi za  Afrika Mashariki katika Uwanja wa Amahoro Nchini Rwanda Tanzania ilishinda 29-27.
Mchezaji  Veronica Patrick wa Tanzania akiwania mpira mbele ya Wachezaji wa Uganda katika michezo wao wa Kwanza wa mashindano ya Majeshi kwa nchi za  Afrika Mashariki katika Uwanja wa Amahoro Nchini Rwanda Tanzania ilishinda 29-27 .
(Picha na Selemani Semunyu).

Na Selemani Semunyu JWTZ.
TIMU ya Mpira wa Pete (Netball) ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania imerejesha heshima yake baada ya Kuwafunga mabingwa Watezi  wa Michuano hiyo kwa Mpira wa Pete Uganda kwa magoli 29 kwa 27.

Katika Mchezo huo uliokuwa wa Vuta nikuvute  na rabsha za hapa na pale zilizizojitokeza kabla wakati na Baada ya Mchezo huo ambao ulikuwa na Upinzani Mkali kutokana na historia ya Timu hizo.

Katika Robo ya Kwanza Tanzania ilimaliza ikiongoza kwa magoli saba kwa Sita huku Timu zote zikicheza Mchezo wa kuviziana lakini uliojaa nguvu na kukamiana miongoni mwa Wachezaji.

Katika Robo ya Pili Tanzania pia ilimalizai ikiwa mbele kwa mabao 13 kwa 11 kukiwa na tofauti ya magoli mawili tofauti na robo ya kwanza ambayo ilimalizika kwa tofauti ya goli moja.

Robo ya Tatu Uganda walikuja na kusawazisha na kasha kuongeza na hivyo kumaliza kwa ushindi wa magoli 20 kwa 19 ya Tanzania  na kuwafanya Tanzania kwenda kujiuliza.

Hatimaye robo ya Mwisho ikamalizika na Timu ya Tanzania kuibuka na Ushindi na hivyo kuwatisha Mabingwa wa mwaka uliopita pengine utarejea kwa Tanzania Kwa Upande wa Nahodha wa Timu hiyo Dorita Mbunda alisema mechi yao na Uganda wamecheza kama fainali kutoka na historian a kuahidi kujipanga kwa ajili ya kuwakabili Kenya. 

Kwa upande wake Nahodha Uganda Lilian Ajio amelalalimika Waamuzi kutoelewa Sheria Mpya za Mchezo huo hali iliyopelekea wakati mwingine kutokuwa na maamuzi sahihi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...