Na Mathias Canal, Dodoma

Maonesho na Mashindano ya mifugo Kitaifa sanjari na Maonesho ya Kilimo yametoa changamoto ya kuleta mapinduzi katika Ufugaji, Uvuvi, na Kilimo na kutoa ajira hususani kwa vijana kuwaongezea zaidi kipato na kuondoa umasikini.

Hayo yamesemwa na Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu-Kazi, Vijana na Ajira Mhe Antony P. Mavunde wakati akifunga maonesho ya wakulima Nane nane Kanda ya Kati Dodoma yaliyokuwa yanafanyika katika uwanja wa Nzuguni kwa kauli mbiu ya "Kilimo, Mifugo na Uvuvi ni nguzo ya Maendeleo, Kijana shiriki kikamilifu (Hapa Kazi Tu).

Amesema kwa kuwa serikali ya awamu ya Tano inayoongozwa na Mhe Rais John Pombe Magufuli inatekeleza azma ya kuhamishia makao makuu mjini Dodoma ameishauri Wizara ya Kilimo, Mifugo, na Uvuvi na ile ya Biashara na masoko kuangalia uwezekano wa kuanzisha rasmi maonesho ya Kilimo, Mifugo, na Uvuvi ya Kimataifa (International Agriculture Trade Fair) katika uwanja wa Nzuguni ambao ndio uwanja wenye eneo kubwa kwa maonesho ya Kilimo hapa nchini.

Aidha ametoa wito kwa Wizara, taasisi/Makampuni ya umma na binafsi, Mabenki na wadau wote wa kilimo na mifugo kuendelea kuwasaidia wakulima na wafugaji hapa nchini ili kuongeza uzalishaji kuwezesha upatikanaji wa malighafi kwa ajili ya viwanda vinavyokusudiwa kuanzishwa.

"Naomba niwaambie wakulima na wafugaji wetu kuwa maonesho ninayoyafunga hii leo ni muafaka na fursa nzuri kwao hususani vijana kwenda kuanza mara moja kutumia mlichojifunza na kuleta mapinduzi yenye maendeleo chanya yanayotarajiwa kiuchumi, hivyo napenda kuchukua nafasi hii kuzikumbusha Halmashauri za serikali za mitaa zote kuwahamasisha wakulima, Wafugaji na wadau wengine kutumia teknolojia zilizooneshwa hapa kuongeza ufanisi wao katika Kilimo, Mifugo na Uvuvi” Alisema Mavunde

Naibu waziri ofisi ya Waziri Mkuu- Kazi, Vijana na Ajira Mhe Antony P. Mavunde (Mb) akisikiliza kwa makini maelekezo ya namna ya kuchakata mihogo kutoka kwa mkulima wa zao hilo tangu mwaka 1980 kutoka Kijiji cha  Nzuguni Josiah Malogo Ndoya
Mhe Mavunde (Mb) akisikiliza kwa makini namna ya kulima mahindi kwa mbinu bora na za kisasa ili kuwa na mavuno yenye tija.
Naibu waziri ofisi ya Waziri Mkuu- Kazi, Vijana na Ajira Mhe Antony P. Mavunde (Mb) akisikiliza maelekezo katika banda la Halmashauri ya Wilaya  ya Chemba kuhusu umuhimu wa matumizi ya dawa katika kilimo cha kisasa 

Mhe Mavunde alipotembelea banda la ushonaji la Jeshi la kujenga Taifa JKT katika Maonesho ya Nane nane kabla ya kuyafunga rasmi 
006 Mhe Mavunde alipotembelea banda la maonesho ya wanyama aina ya mbuzi, Ng’ombe na Kondoo la kampuni ya Ranchi za taifa (NARCO LTD) .

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...