THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

Gadget

This content isn't available over encrypted connections yet.

MBUNGE ULEGA AENDELEA NA ZIARA YAKE YA KUSIKILIZA NA KUTATUA MATATIZO YA WANANCHI JIMBONI KWAKE MKURANGA MKOANI PWANI

 Mbunge wa Jimbo la Mkuranga Abdallah Ulega akiwa na baadhi viongozi wa vijiji wakielekea eneo lengine kukutana na wananchi na kuyasikiliza na kutatua matatizo yao kwa namna moja ama nyingine wilayani Mkuranga,mkoa wa Pwani
 Mbunge Abdallah Ulega akijionea hali halisi ya miundombinu ya usafiri kwa wananchi wake wa Mkuranga mkoani Pwani
 Mbunge wa Jimbo la Mkuranga Abdallah Ulega akizungumza na  wananchi wa kijiji cha Kurutu kilichopo kata shungubweni wilayani Mkuranga katika ziara zake za kushukuru wanakijiji hao Kwa kumchagua kuwa mbunge wao.
 Shabani Omary  akiuliza swali kwa mbunge wa jimbo la mkuranga Abdallah Ulega leo mkoani Pwani
 Mbunge wa Jimbo la Mkuranga Abdallah Ulega akizungumza na walimu wa shule ya  msingi  kijiji cha Kurutu kilichopo kata ya shungubweni  leo mkoani Pwani.

wananchi wa kijiji cha Kurutu kilichopo kata shungubweni wilayani Mkuranga wameshauliwa kuchukua shamba lenye ukubwa wa hekari 66.6 ambalo alipewa mwekezaji Salim tangu mwaka 1988 na kushindwa kuliendeleza,ili walitumie Kwa shughuli za kuzalisha mali.

Ushauri huo ulitolewa wilayani humo na Mbunge wa jimbo hilo Abdallah Ulega mara baada ya kupokea malalamiko Kutoka Kwa wananchi wake akiwa katika ziara zake za kushukuru wanakijiji hao Kwa kumchagua kuwa mbunge wao.

Ulega alisema haiwezikani watu wanajimilikisha mashamba makubwa miaka hadi miaka alafu wanashindwa kuyaendelea huku wananchi wakipata shida ya kukosa maeneo hata ya kulima kilimo cha mbogamboga vijana.

"Nasema kuwa kama shamba hilo limekaa miaka yote hiyo haliendelezwi, napia huyo mwekezaji haonikani sasa mnasubiri nini kulichukua na kufanya uendelezaji,nashauri litwaeni alafu tutapambana nayo huko mbele"

Pia Ulega aliwaeleza wananchi hao kuwa siasa imekwisha na kilichobaki ni watu kufanya Kazi Kwa nguvu zote na kwamba atakuwa bega Kwa bega katika kuhakikisha maendeleo wanayapata Kwa haraka.

Awali wananchi wa kijini cha Kurutu walimweleza mbunge kuwa wanashamba kubwa ambalo alipewa mwekezaji miaka mingi iliyopita tena kienyeji lakini hadi leo ameshindwa kuliendeleza hivyo awasaidie walipate ili vijana wa eneo hilo wazalishe chumvi.

Mbunge huyo bado anaendelea na ziara zake za kutembelea kijiji hadi kijiji kwa lengo la kuwashukuru na kuhimiza shughuli za maendeleo ambapo anawataka kujituma katika kufanya kazi kwani wilaya hiyo imechelewa kimaendeleo.