Mbunge wa jimbo la Mkuranga Abdallah Ulega amezindua kisima cha Maji katika kijiji cha Mwalusembe ,ambacho kimejengwa katika shule ya msingi muongozo Kwa ufadhili wa Taasisi ya Afraca Reflection Foundation
 
Mara baada ya uzinduzi huo,Mh. Ulega aliwashukuru wafadhili hao na kuwaomba kuendelea kusaidia wilaya hiyo ili kukabiliana na uhaba wa Maji uliopo na kuwa Wilaya ya Mkuranga ni moja ya maeneo ambayo yanachangamoto kubwa ya Maji.
 

Mh.Ulega Pia aliwataka wananchi wa kijiji hicho kutumia Maji hayo vizuri ikiwa pamoja na kulinda miundombinu yake ikiwamo solar na vinginevyo ili visiibiwe,Mh Ulega tangu kuchaguliwa kwake kuwa Mbunge wa jimbo hilo tayari ameshachimba visima katika vijiji zaidi ya vitano huku akisaidia kutatua mbalimbali ya wananchi ambayo yamekuwa kero kwao.

Mbunge wa Jimbo la Mkuranga,Abdallah Ulega akizungumza na wananchi wa kijiji cha Mwalusembe kweye hafla ya uziduzi wa kisima cha Maji katika kijiji cha Mwalusembe, ambacho kimejengwa katika shule ya msingi Muongozo kwa ufadhili wa Taasisi ya Afraca Reflection Foundation leo mkoani Pwani. 
.Mbunge wa jimbo la Mkuranga Abdallah Ulega akizindua kisima cha Maji katika kijiji cha Mwalusembe ambacho kimejengwa katika shule ya msingi muongozo Kwa ufadhili wa Taasisi ya Afraca Reflection Foundation leo mkoani Pwani.

Mbunge wa jimbo la Mkuranga, Abdallah Ulega akiwasil katika kijiji cha Mwalusembe kwa ajili ya kuziduzi kisima cha Maji ambacho kimejengwa katika shule ya msingi Muongozo mkoani Mpwani.
(Picha na Emmanuel Massaka,Globu ya jamii).

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...